10 September 2012

Washiriki EBSS kazi ipo


Na Mwandishi Wetu

WASHIRIKI 50 bora kutoka mikoa mbalimbali wanaoshiriki katika shindano la Epiq Bongo Star Sarch (EBSS), jana walitarajiwa kuchuana katika mchujo uliofanyika katika Kituo cha ITV katika kuwania sh. milioni 50.

Washiriki hao watachujwa kutoka 50 hadi kufikia 20, wataonesha uwezo  wao mbele ya majaji wa kuimba pamoja na kuvutia wakiwa jukwaani.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti tofauti Dar es Salaam juzi, wawakilishi kutoka kila mkoa walikuwa na nafasi ya kuelezea namna ambavyo wamejipanga kuhakikisha kuwa wanawakilisha mikoa yao vema.

Mshiriki wa Mkoa wa Dar es salaam, Sixmon Mdeka (Albino)    aliyeonekana kujiamini zaidi tangia siku ya mwanzo alisema kuwa atatumia ufundi wake wa kuimba nyimbo za miondoko ya reggae pamoja na nyimbo za miondoko tofauti tofauti.

Naye mshiriki ambaye ni Mwanafunzi wa shule ya Sekondari ya Makongo, Husna Nasoro alisema  atahakikisha kuwa anaziimba vema nyimbo za wasanii wa kike akiwamo Linah ambae kwake anamuona kama ndio mfano wake wa kuuiga katika muziki.

Pia  washiriki kutoka mkoa wa Arusha nao walisisitiza kuwa watahakikisha kuwa wanaondoa mtazamo kuwa jiji hilo limebobea katika Hip Hop tu ambapo wataimba nyimbo mbalimbali.

Akizungumzia usaili huo wa kuwachuja,  Jaji Mkuu wa shindano hilo, Ritha Paulsen alisema kwa sasa ndio mchakato wa mchujo unamalizika na wanaanza kazi yenyewe ya kuwapatia wapenzi wa EBSS burudani safi zaidi.

No comments:

Post a Comment