06 September 2012
Washindi wa 'Vuta Mkwanja' wazawadiwa
Na Mwandishi Wetu, Moshi
KAMPUNI ya vinywaji ya Coca-Cola, Bonite jana imewazawadia fedha taslimu washindi wengine 16 wa promosheni ya 'Vuta Mkwanja', ambayo ilianza Julai mwaka huu na inatarajiwa kumalizika mwezi huu.
Washindi hao ni Fredy Charles mkazi wa Mianzini, Arusha, Hamid Nkya (Ngaramtoni Arusha) na Rahim Hashim (Majengo, Moshi) ambao kila mmoja ameshinda sh. milioni moja.
Waliobahatika kushinda sh. 100,000 ni Goodluck Kessy (KCMC, Kitandu), Focus Njau (Uchira, Moshi), Joseph Kauwedi (Lyamungo Sec, Moshi), Samson Mushi (Kiusa, Moshi), Fatuma Ibrahim (Babati) na Narender Mushi (Moshi mjini).
Wengine ni Julius Michael (Sakina, Arusha), Christina Kessy (Arusha), Dorin Massawe (Arusha), Khadija Said (Kijenge, Arusha), Lucas Tito Sumari (Makumira), Magdalena John (Kimandolu, Arusha) na Lilian Maro (Ngaramtoni, Arusha).
Akizungumza baada ya kukabidhiwa zawadi yake, mmoja wa washindi wa sh. Milioni moja, Hamida Nkya ambaye ni mwalimu wa Shule ya Sekondari Mringa iliyopo Ngaramtoni, Arusha alisema anajisikia furaha kupata bahati ya kuwa mshindi.
"Siku ya leo (jana), ninayo furaha sana, nilikunywa soda nikaangalia chini ya kizibo nikakuta nimejishindia milioni moja. Nilikuwa na ndota ya siku nyingi ya kuanzisha mradi wa kufuga kuku na tatizo ilikuwa ni mtaji.
Akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi hizo Meneja Masoko wa Bonite Bottlers, Christopher Loiruk alitoa wito kwa wateja wa kampuni yake kuendelea kunywa soda zao pamoja na jamii kuibuka washindi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment