14 September 2012

Wasanii watakiwa kujiheshimu



Na Zourha Malisa

WASANII wameshauriwa kujiheshimu  na kuwa na heshima  juu ya kazi zao za sanaa ya muziki ili waweze kufikia malengo waliyojiwekea.

Tuhuma za kila siku kwenye baadhi ya vyombo vya habari haziwezi kumjenga msanii katika soko la muziki la kimataifa bali inachangia  kumbomoa na kuvunja heshima yake kwa wadau na mashabiki wake wa muziki .

Wasanii wanatakiwa kuwa na uongozi utakaowaongoza na kuwapa mafunzo nini maana ya sanaa ili waweze kuheshimu kazi zao

Kauli hiyo ilitolewa na Msanii anayetikisa katika anga za muziki wa kizazi kipya nchini, Barnabas Elias ‘Barnaba’alipokuwa akieleza kuhusu uzinduzi wa  staili yake mpya ya uimbaji inayoambatana na muonekano wa mavazi pamoja na aina ya nywele .

Alisema kuwa mashabiki wake watarajie kumuona Barnaba kuwa tofauti kuanzia mavazi mpaka uimbaji hii yote katika kuboresha kazi ili zionekane zina ubora .

Aliongezea kuwa kwa kuwa anaheshimu kazi zake pamoja na kuwajali mashabiki wake hufikiria vitu vyenye ubora zaidi katika kazi zake.

No comments:

Post a Comment