14 September 2012

Maoja atamba kumchapa Mnamibia



Na Mwali Ibrahim

BONDIA Rajabu Maoja amejinadi kuhakikisha anarudi na ushindi katika pambano lake la ubingwa wa IBF dhidi ya Mnamibia, Gottlieb Ndokosho katika pambano linalotarajiwa kufanyika Septemba 29, mwaka huu katika jiji la Windhoek, Namibia.


Akizungumza kwa simu kutoka mkoani Tanga, alipoweka kambi, Maoja alisema, katika pambano hilo lilopewa jina la 'Vita ya Jangwa la Kalahari' amejipanga kuhakikisha anawapa raha watanzania kwa kurudi na ubingwa kwani ana imani atarudi nao.

"Niko huku Tanga ambapo ndio nyumbani lakini pia ndipo nilipoweka kambi yangu hadi siku nitakayo kwenda katika shindano, nimejipanga kuhakikisha nanyakua ubingwa ikiwa ni pamoja na kuitangaza nchi kwani rekodi yangu ni nzuri tofauti na ya mpinzani wangu  na nimejiandaa vizuri kipindi chote tangu nipate taarifa ya pambano hili," alisema.

Pambano hilo litasimamiwa na Rais wa IBF katika Bara la Afrika, Mashariki ya Kati, Ghuba ya Urarabuni na  Ghuba ya Uajemi, Onesmo Ngowi huku akishirikiana na Bodi ya ngumi na mieleka ya Namibia.

Naye kwa upande wake Ngowi alisema, Mapambano hayo yanayotambuliwa na IBF yako katika mpango  wa programu ya “Utalii wa michezo” ambao IBF na USBA umeufadhili na kuuendesha katika bara la Afrika huku Tanzania na Ghana zikiwa ni nchi za majaribio katika mpango huo.

Aliongeza kuwa Programu hiyo itawapa mabondia wengi wa Kitanzania nafasi nyingine kugombea mikanda ya IBF sehemu mbalimbali Duniani na kuitangaza ya Tanzania.

No comments:

Post a Comment