18 September 2012

Walimu Ilala Boma watakiwa kuendeleza michezo



Na Heri Shaaban

WALIMU wa wanafunzi wa Shule ya Msingi Ilala Boma, wametakiwa kuendeleza kitengo cha taaluma cha michezo katika  shule hiyo, ili kuibua wanafunzi wenye vipaji washiriki mashindano ya taifa.


Ushauri huo umetolewa Dar es Salaam jana,katika mahafali ya darasa la saba ya shule hiyo na Diwani wa Viti Maalum Wanawake Ilala,Batuli Mziha wakati wa kutoa hotuba yake.

Batuli alisema  kamati ya michezo ya shule hiyo ikisimamia vizuri kitengo michezo katika shule hiyo, kutakuwa na wachezaji wazuri watakaoshiriki mashindano ya ngazi ya mkoa hadi taifa,

Aliwaagiza wazazi na kamati ya shule washirikiane katika kukuza michezo ya shule hiyo, ili kuweza kuisadia serikali iweze kupata vipaji vya watoto wa shule za msingi.

Alisema katika sekta ya michezo inatakiwa kuweka mbele zaidi vitu viwili elimu na michezo, ili wachezaji waweze kusonga mbele hivyo wasijitume katika suala moja.

No comments:

Post a Comment