18 September 2012

Kamati Miss Tanzania kuwafunda wanyange wa Temeke



Na Mwandishi Wetu

KAMATI ya Miss Tanzania leo inatarajiwa kutembelea kambi ya Redd’s Temeke 2012,  kwa ajili ya kuwafunda vimwana hao kutoka vitongoji vya Kigamboni, Kurasini na Chang’ombe, kuhusu mambo mbalimbali ndani ya mashindano ya urembo.


Kamati hiyo itaongozwa na Mkurugenzi wake, Hashim Lundenga atakayefuatana na mshauri wa masuala ya urembo katika kamati yao, Dk. Ramesh Shah, Katibu Bosco Majaliwa, Mkuu wa Itifaki, Albert Makoye na Mjumbe wa kamati hiyo, Lucas Rutta.

Shindano la Redd’s Miss Temeke, linafanyika Ijumaa hii katika ukumbi wa PTA (SabaSaba Hall) na tiketi za VIP zimeshaanza kuuzwa katika klabu za City Sports Lounge iliyopo makutano ya Samora na Azikiwe na Nyumbani Lounge iliyopo maeneo ya Namanga ambapo VIP kwa mtu mmoja ni sh. 50,000 , na endapo mtu atataka kununua meza moja ya watu nane atalipia sh.400,000.

Warembo hao ni Agness Goodluck, Angela Gasper, Flaviana Maeda,Edna Sylvester, Catherine Masumbigana, Khadija Kombo, Neema Doreen, Flora Kazungu, Lilian Joseph, Elizabeth Peter, Elizabeth Boniphace, Jesca Haule, Zulfa Bundala, Mariam Ntakisivya na Esther Albert.

Mbali ya vinywaji vya Redd’s  na Dodoma Wine, Miss Temeke pia imedhaminiwa na gazeti la Jambo Leo, katejoshy.blogspot.com, Mariedo Boutique, Push Mobile, City Sports Lounge, 100.5 Times FM, Kitwe General Traders, Global Publishers na 88.4 Cloud’s FM.

Shindano hilo litakuwa ni miongoni mwa mashindano ya lala salama kabla ya kupata warembo watakaoungana na warembo wa kanda nyingine kuingia kambini kumtafuta mrembo wa Redds Miss Tanzania kwa Mwaka huu.

No comments:

Post a Comment