17 September 2012
Waamuzi nchini wazidi kutupiwa lawama
Na Speciroza Joseph
KOCHA timu ya African Lyon, Pablo Velez amekubali kubeba lawama za kupoteza mchezo wao wa kwanza wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Simba kwa kusema mwamuzi wa mchezo huo hakuwa sahihi katika maamuzi yake.
Lyon juzi aliikaribisha ligi kwa kupokea kipigo cha 3-0 kutoka kwa bingwa mtetezi, Simba na kuiacha timu hiyo ikijiuliza ligi itakwendaje.
Baada ya kumalizika kwa mchezo huo uliopigwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Velez aliyeingia mkataba na timu hiyo mwezi uliopita, alisema wamefungwa kutokana na sababu za kiufundi na mwamuzi pia alichangia.
Alisema mwamuzi alionesha upungufu kwa kushindwa kutoa maamuzi sahihi na kuiumiza timu yake, mechi hiyo ilikuwa chini ya mwamuzi Oden Mbaga wa Dar es Salaam.
Akizungumzia maandalizi ya mechi hiyo, alisema walijiandaa vizuri kucheza na Simba na kuwaelekeza wachezaji wake jinsi ya kukabiliana na mbinu za Simba za kupata penalti lakini wachezaji walijisahau na kuruhusu kufanya kosa hilo.
Alisema kupoteza mchezo huu wa kwanza kwao sio sababu ya wao kukata tamaa zaidi watajifunza na kurekebisha makossa yao ili wafanya vizuri katika michezo ijayo.
Mmiliki wa African Lyon, Zamunda amelalamikia kitendo cha wachezaji wake kukataliwa kuvaa jezi zenye nembo ya mdhamini wao mpya kampuni ya simu za mikononi ya Zantel na kuita kitendo hicho kuwa ni unyanyasaji.
Lyon juzi waliingia makubaliano ya kampuni hiyo kuwa mdhamini wao na kutangaza jezi zao zenye nembo ya kampuni hiyo, huku ligi kuu ikidhaminiwa na kampuni nyingine ya mtandao ya simu za mkononi ya Vodacom.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment