17 September 2012
Mabondia Ruvuma kamili mashindano ya Taifa
Na Mhaiki Andrew, Songea
TIMU ya Ngumi ya Mkoa wa Ruvuma, juzi imeangwa kwa ajili ya kushiriki mashindano ya mchezo huo ya Taifa na kukabidhiwa vifaa vyenye thamani ya sh. milioni 7.5.
Baadhi ya vifaa hivyo ni grovu, nguo za mazoezi, hard gaurd na jozi 12 za viatu.
Halfa fupi ya kuiaga timu hiyo ilifanyika kwenye Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Songea, Joseph Mkirikiti ambayo ilihudhuriwa na mkuu huyo wa wilaya na wadau wa michezo pamoja na Mwakilishi kutoka Kampuni ya Mantra, Meneja Uhusiano ya jamii, Benard Mihayo.
Akizungumza kabla ya timu hiyo kuagwa, Mkuu wa Wilaya hiyo, Mkirikiti aliwakumbusha mabondia hao watumie uzalendo na uhodari wao katika mchezo huo kuutangaza Mkoa wa Ruvuma kama ilivyo kwa fursa nyingine za sekta za utalii wa ndani katika kujitoa kimaisha.
Alisema mchezo huo wa ngumi unaweza kumtoa kijana kimaisha kama atakuwa anajifahamu kuwa anachokifuata huko ni kitu gani kama ilivyokuwa kwa bondia Rashid Matumla ambaye alijitangaza vizuri.
Naye Mwakilishi wa kampuni ya Mantra, Mihayo alisema kampuni yao pamoja na kujihusisha na uchimbaji wa madini ya urenium bado wamekuwa mstari wa mbele kuendeleza michezo mkoani Ruvuma na alidai michezo ni sehemu ya maisha katika kuibua vipaji na wakaendeleza maisha yao.
Aliwataka watumie vifaa hivyo katika kuutangaza mkoa huo na waachane na vishawishi ambavyo vinaweza kuwapotezea uaminifu kwa kujikuta wanashawishika kwa lengo la kujipatia fedha.
Kwa upande wa Mwenyekiti wa ngumi mkoani humo,Sikitiko Komba aliishukuru kampuni hiyo na kuahidi vifaa hivyo vimewapa molari mabondia wao kuhakikisha wanajizolea medali nyingi na kuwa historia kwa mkoa kama ilivyo kwa upande wa soka katika miaka ya nyuma
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment