05 September 2012
UVCCM yawaonya wapigadebe
Na Anneth Kagenda
UMOJA wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Mkoa wa Dar es Salaam, umewahadharisha viongozi wa chama hicho wenye tabia ya kuwapigia debe baadhi ya wagombea katika chaguzi ambazo zinazoendelea ndani ya chama waache mara moja.
Kama umoja huo utawabaini viongozi wa aina hiyo, utachukua hatua za kisheria dhidi yao ili iwe fundisho kwa wengine.
Mwenyekiti wa umoja huo mkoani hapa, Bw. Said Mtimizi, alisema hakuna kiongozi anayeruhusiwa kuwabeba watu wala kuingilia uchaguzi wao ambao unawahusu vijana.
“Vijana waachwe wafanye chaguzi zao bila kuingiliwa na viongozi,
wale waliomaliza muda wao wakae pembeni, kuna tatizo ambalo limejitokeza chaguzi hizi la majina mengine kutorudi kutokana na wagombea kuwa na umri mkubwa.
“Suala hili ni la kikanuni hivyo hawezi kulipinga, tunawashangaa waliovunja uchaguzi Kinondoni kwani kila mtu ana wakala wake, chanzo cha vurugu ni masilahi binafsi lakini tumejipanga kulimaliza ambapo kila mgombea atahesabiwa kura zake,” alisema.
Kwa upande wake, Katibu wa UVCCM, mkoani hapa, Bw. Omary Ng'wanang'walu, alisema mara baada ya kutoa taarifa za nani aliyesababisha vurugu, watamuita na muhuhoji.
Alisema kasoro zake zitajadiliwa na wengine ambao wataonekana kuwa na makosa wataambiwa haata kuhamishwa katika nafasi walizopo ili kulinda heshima ya chama.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment