10 September 2012

Uchaguzi Wazazi Taifa CCM walalamikiwa


Na Mwandishi Wetu

UCHAGUZI wa Mwenyekiti wa Jumiya ya Wazazi Taifa ambao umefanyika jana jijini Dar es Salaam, unadaiwa kuingia dosari kwa madai ya ukiukwaji kanuni ambazo zinazuia wagombea wenye kazi za kudumu kutorohusiwa kugombea nafasi hiyo.


Imeelezwa kuwa, hatua ya Baraza la Utekelezaji kupitisha majina ya mengi ya wabunge, imewahuzunisha na kuwakasirisha wanachama wa jumuiya hiyo ambao wanamtaka Mwenyekiti ambae atakua nao muda wote.

Akizungumza na gazeti hili kwa sharti la kutoandikwa jina, mmoja wa Wajumbe wa Mkutano Mkuu Wazazi Taifa, amehoji hatua ya baraza hilo kuvunja kanuni zake kwa kupitisha majina saba ya wagombea badala ya matatu wengi wao wakiwa wabunge.

Waliopitishwa katika uchaguzi huo ni Bw. Nimrodi Mkono, Bi. Martha Mlata, Bw. Said Bwanamdogo, Dkt. Norman Sigalla, Bw. Abdallah Bulembo na Bw. Daniel Machemba, Bw. Barongo Rweikiza.

“Naiomba Kamati Kuu ya CCM, kutowateua wabunge kugombea Uenyekiti wa jumuiya hii kwa sababu wana kazi ya kudumu pamoja na shughuli nyingine,” alisema.

Alisema kuwateua wabunge hao ni kudhoofisha jumuiya hiyo na kuikosesha kiongozi ambaye atasikiliza matatizo yao muda wote.

No comments:

Post a Comment