12 September 2012

Tunalaani vurugu za vyama vya siasa-UWT



Na Pendo Mtibuche, Dodoma

UMOJA wa Wanawake Tanzania (UWT), umelaani vurugu ambazo zinadaiwa kufanywa na baadhi ya vyama vya siasa na kuvuruga amani iliyopo hivyo wamemuomba Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Bw. John Tendwa, kuvichukulia hatua.


Katibu wa umoja huo, Bi. Amina Makilagi, aliyasema hayo mjini Dodoma jana baada ya kumalizika mkutano wa siku mbili wa Baraza la Wanawake Taifa.

Alisema ndani ya miaka minne, umoja huo umekuwa ukilaani siasa zinazochochea vurugu, kuvuruga amani ya nchi na kumwaga damu.

“Kwa kweli umoja wetu kupitia kikao tulichokaa hapa Dodoma, tumefikia azimio la kumwambia Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Bw. Tendwa kuhakikisha anachukua hatua kwa wanasiasa uchwara wanaofanya siasa chafu zenye kuleta machafuko,” alisema.

Aliongeza kuwa, siasa za aina hiyo zinaweza kuvuruga amani ya nchi pamoja na kuleta madhara kwa watoto ambao ndio Taifa la kesho hivyo wanahitaji malezi bora na siasa safi ili waweze kuwa na uzalendo wa kuitumikia nchi yao na kukuza uchumi.

Bi. Makilagi alisema jambo kubwa ambalo lilijadiliwa katika kikao hicho na kutolewa maamuzi ni suala la afya ya mama na mtoto ambapo UWT imetoa tamko la kuishauri Serikali kujipanga na kuboresha mazingira ya sekta hiyo ili kuokoa vifo vinavyotokea.

Alisema jambo jingine wanalokusudia kulifanya ni kumpngeza Dkt. Asha Rose Migiro kwa heshima aliyowapa wanawake wa Tanzania ambapo hafla hiyo itafanyika Septemba 15 mwaka huu, jijini Dar es Salaam na itahudhuriwa na wanawake kutoka mikoa tofauti.

3 comments:

  1. Ayooo! Tungeshangaa kama UWT wangelaani vitendo vya serikali ya CCM (ambacho ni chama mama cha UWT)vya kutumia polisi kuua raia wasio na hatia wakiwa katika harakati za kisiasa zinazoongozwa na vyama vya upinzani. UWT wana upofu wa kisiasa.Wanajua kuwa kudidimia kwa CCCM ndio mwisho wao pia. Ebu wajiulize swali hili dogo: KAMA WANAOUAWA KILA UCHAO WANGEKUWA WANACHAMA AU MASHABIKI WA CCM, WAO (UWT)WANGEINGIA BARABARANI KUSHANGILIA MAUAJI HAYO? au,swali jingine dogo zaidi: KAMA MIKUTANO YA HADHARA YA CCM INGEZUIWA KWA VISINGIZIO VYEPESI VYA POLISI, AU KIPIGWA MABOMU YA MACHOZI, AU KUZINGIRWA NA FFU WALIOVALIA KIVITA KILA UCHAO, WANGEOMBA WAKUU WA SHERIA, MSAJILI WA VYAMA VYA SIAASA NA SAIDI MWEMA WAPANDISHWE VYEO KWA UMAHILI WAO WA KUWEKA MAZINGIRA SAWA KWA VYAMA VYOTE VYA SIASA KUFANYA SIASA ZA VYAMA VINGI BILA UBAGUZI? Kuna m-UWT yeyote anayeweza kujibu maswali hayo madogo kwa ukweli? Wanyamaze tu! Wao ni vipaza sauti vya CCM na serikali yake.Hatutawalaumu.Wasubiri SUNAMI ya NGUVU YA UMMA.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Umesema kweli hii nchi ni yetu sote hakuna anayefurahia mauaji.Lakini haya ni matokeo ya Uongozi mbovu tulionao .Hii ni nchi ya vyama vingi, nadhana dhana hii kwa wenzetu ni ya kinadharia tu hivyo ndiyosababu tuna ona haya yakitokea

      Delete
  2. Bi. Amina ukisema wanasiasa uchwara unawazungumzia CCM tena ukae kimya kabisa mabosi wako wasikufukuze kazi.Unakumbuka fisadi moja lilipowabeza kabla ya kujitoa ubunge na kuachia nafasi zote ndani ya chama chako,lilisema kwa jeuri kwamba LINAACHANA NA SIASA UCHWARA za CCM.Sasa bibi unataka Tendwa awachukulie hatua wanasiasa wa CCM,atakula wapi? Basi kama anaweza angalau aanze na Bw.Nchimbi!

    ReplyDelete