10 September 2012

Shomari Fungo popote ulipo na huyu dadako



Na Rehema Maigala

MSICHANA Neema Shomari Fungo (20)Mkazi wa Mbagala Kizuiani Dar es Salaam anamtafuta kaka yake Mohamed Shomari Fungo ambaye hajawi kumuona hata siku moja.

Akizungumza katika ofisi za gazeti la hili, msichana huyo alisema kuwa kwa hivi sasa anaishi na baba yake mdogo Bw.Jeikan Fungo na kwamba wazazi wake wote wawili wameshafariki dunia.

Alisema kuwa enzi za uhai wa baba yake alishawahi kumwambia kuwa ana kaka yake ambaye wamechangia baba kwa wakati huo alikuwa anaishi Iringa, lakini sasa hivi hajui anaishi wapi.

"Ninahamu ya kumjua kaka yangu kwani sina ndugu yangu mwingine yeyote niliokuwa nawajua tayari wameshafariki ninaomba kaka yangu ajitokeze ili tuweze kufahamiana,"alisema

Bi. Neema alisema kuwa kwa sasa anatarajia kwenda kujiunga na Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM)baada ya matokeo yake ya kidato cha sita kutoka vizuri.

Alisema kuwa amemtafuta kwa njia mbalimbali bila ya kupata mafanikio yeyote hivyo ameamua kujitoa katika gazeti ili aweze kumpata kaka yake kwa urahisi.

Kwa mawasiliano zaidi anaweza kutumia namba hizi na kunipata kwa urahisi 0657-477435 au 0617-960665.

No comments:

Post a Comment