18 September 2012

SBC yazindua shindano la Tajirika na Pepsi



Leah Daud na Jesca Kileo

KAMPUNI ya SBC Tanzania Ltd, jana imefanya uzinduzi rasmi wa shindano la “Burudika, Tajirika Zaidi na Pepsi”, ili kuboresha maisha ya Watanzania.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es salaam jana, Meneja Mauzo wa kampuni hiyo, Bw. Rashid Chenja, alisema shindano hilo linashirikisha soda aina ya Pepsi, Mirinda, Mountain Dew (300ml), na Seven Up (350ml).

Alisema shindano hilo litakuwa na zawadi za fedha taslimu sh. 10,000, 5,000, soda za bure na sh. milioni 1.5 ambazo mshindi atalazimika kwenda Makao Makuu ya kampuni hiyo.

Aliongeza kuwa, zawadi hizi zipo kwenye vizibo ambapo SBC inawatambua mlinda mlango wa Simba, Juma Kaseja na Barnaba Elias kama mabalozi wao wa kutangaza bidhaa za Pepsi 2012/13.

“Mabalozi hawa watatumika katika shughuli mbalimbali za jamii kwani kampuni yetu imekuwa ikijihusisha na kandanda pamoja na muziki kwenye kampeni zetu hivyo tumeamua kuwatumia nyota wa Tanzania kama mabalozi,” alisema Bw. Chenja.

Alitoa wito kwa Watanzania wote kutumia fursa hiyo kuburudika, kutajirika zaidi na Pepsi kwa kuwa milionea.

No comments:

Post a Comment