18 September 2012
Msingi wa haki za binadamu ufuatwe
Na Jesca Kileo
HAKI za binadamu ni mahitaji aliyonayo kila mtu ambayo yakitimizwa humuwezesha kuishi maisha yenye hadhi, amani na upendo.
Haki hizi zimeorodheshwa hasa katika azimio la ulimwengu la haki za binadamu lililotolewa na Umoja wa Mataifa mwaka 1948 na kuendelea kwa miaka kadhaa badae.
Miongoni mwa haki hizo ni pamoja na haki ya kuishi
kuchagua kazi, kutokuwa mtumwa, kuwa na mali, kutoa maoni yake kwa uhuru kuwa salama, kutotishwa, kuwa na kinga dhidi ya hatua za kisheria, pamoja na nafasi ya kupinga kwa njia halali kutokamatwa kwa kosa la mtu mwingine.
Pia, kupewa nafasi ya kujitetea mbele ya mahakama, kutazamiwa kuwa mtuhumiwa bila ya hatia kabla mahakama haijatoa hukumu, kuwa na uraia wa nchi fulani, kupiga kura katika uchaguzi huru, kupewa kimbilio kama nchi asilia inazuia uhuru wa msingi na kuchagua dini na kuishi kufuatana na dini.
Nyingine ni kupinga pamoja na wengine maazimio ya serikali kwa njia ya amani, kupata elimu, kufunga ndoa na mtu mzima yeyote.
Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na raia wake wote wanabanwa na haki ya watu kufanya kazi zinazosaidia jamii kwa uhuru bila kuzuiliwa na mtu yoyote.
Mfumo mzima wa utoaji wa haki nchini bado upo nyuma na matokeo yake kunakuwepo na mauaji mengi yanayotokea mara kwa mara kutokana na tabaka la watu wenye nacho kuwakandamiza wasiokuwa nacho.
Serikali imekuwa ikiwabana raia wake kutozungumza ukweli kuhusu jamii fulani, taasisi, shirika au hata ya mtu binafsi imekuwa ikijali zaidi maslahi kuliko utu wa mtu.
Kuna haki za msingi za binadamu kama vile kujielezea au kuelezea tukio lililoshuhudiwa, lakini limekuwa halifuatiliwi nchini kwasababu mtu ukieleza tukio uliloliona unaweza ukachukuliwa sheria kwakusema ukweli wa jambo fulani.
Mfano mzuri kuna mwandishi aliripoti kitendo cha kinyama alichofanyiwa mwananchi, cha kushangaza yule mwandishi alikatazwa kuripoti lile tukio na kuonywa kuwa endapo akiendelea atapandishwa kizimbani.
Hapa hakuna uhuru wa kuongea wala wa habari maana kama mtu anazuiliwa kuripoti unyanyasaji unaotokea katika jamii fulani kutoka kwa jamii ya watu wa aina fulani, hii ni kuzuiliwa kutimiza haki za watu za msingi.
Uhuru hamna tena ndani ya nchi yetu, waandishi wamekuwa wakipokea vitisho kutoka kwa baadhi ya watu kwasababu tuu wanaripoti habari zao mbaya wanazowafanyia raia ambao hawana pa kuelezea.
Viongozi mbalimbali wamekuwa wakihimiza waandishi wa habari kufanya kazi kwa bidii bila kujali ni mtu wa aina gani amekiuka maadili au kafanya kitendo cha ajabu ambacho sio haki ya binadamu.
Lakini wamekuwa mstari wa mbele kuwahukumu na kuwapa vitisho wale wanaoripoti maasi wanayoyafanya, jambo ambalo ni la kiunafiki.
Mwaka kuna gazeti limefungiwa kwasababu ya habari inayoendelea kutokea ikionekana kama ni ya uchochezi kwasababu waliripoti kwa undani zaidi wa tukio ambalo lilikuwa limetokea.
Nionavyo, waandishi au vyombo vya habari havitakiwi Tanzania wamiliki waambiwe, kuliko ya kukatazwa kuandika habari na kupata vitisho, ili tuangalie itakuwa nchi ya namna gani bila ya waandishi au vyombo vya habari.
Hamna sababu yoyote ya kufungia gazeti au kutoa vitisho kwakuripoti tukio la kweli lililoitokea na ambalo sio uchochezi, maana bila hivi jamii itakuwa haijui nchi inakwendaje.
Kuna mwanasheria mmoja wa serikali alisema kwamba tatizo kubwa tulilonalo ni usimamizi wa sheria na pia uwezo wa kuendesha mashtaka vizuri bila kuangalia upande wowote au hadhi ya mtu haupo.
Aliendelea kusema kuwa kwa upande wa polisi uwezo wa kung'amua na kukamata wahalifu bado kuna changamoto maana kuna watu wamefanya makosa madogo na kwa bahati mbaya ila wanaozea magereza na wapo waliotenda makosa makubwa na kwa makusudi na wapo mtaani wakiendelea kula maisha.
Mfano akasema kuwa si vizuri kumzungumzia marehemu lakini alimtolea mfano akasema kuna kigogo wa chama fulani enzi za uhai wake aliwahi kuua kwakukusudia lakini ilionekana ameua kwakutokusudia kwasababu ya cheo alichokuwanacho.
Hali ambayo ilipelekea hisia mbalimbali kwa raia kwa wakati ule, jambo hili la mauaji linaonekana kwasasa limeanza tena kwa kasi mpya.
Takwimu zilizofanywa kuanzia januari hadi Septemba mwaka huu zinaeleza kuwa idadi ya vifo vya kukusudiwa ni watu 22 vilivyotokana vilitokea mikononi mwa watu ambao wamepewa jukumu la kulinda na vingine vikishinikizwa na jamii.
Kesi zikifikishwa sehemu husika, raia wanaelezwa kwamba walikuwa wakituliza ghasia ndiyo maana ikatokea hivyo, kitu ambacho sio kweli kwasababu kutuliza ghasia sio lazima uue kwanza au umpige mtu.
Haki ya binadamu hapa iko wapi jamani? Kama watu mkifanya jambo fulani la heri mnachinjwa kama wanyama, hamna haja ya kuwekwa haki za binadamu wala kuitwa binadamu tena.
Nionavyo Kituo cha haki za binadamu na mahakama hazifanyi kazi zake vizuri kwakuzingatia maadili na kanuni za kazi kama inavyostahili, waache kuangalia aina ya mtu anaetenda kosa au ana hadhi gani.
Wahusuka, nawaomba muangalie utu zaidi jamani msiangalie maslahi na mfuatilie kwa undani ukiukwaji wa haki za binadamu unaofanywa na baadhi ya watu.
Tujali zaidi utu kuliko maslahi na mahakama iwawajibishe wote watakaonekana kukiuka haki za binadamu ipasavyo bila kuangalia ni nani amekiuka haki hizo.
Kila binadamu ana haki ya kuishi na kueleza hisia zake.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment