24 September 2012

Rasilimali zilizopo zitumike kuleta maendeleo - Migiro


Na Jesca Kileo

WITO umetolewa kwa Watanzania kutumia rasilimali zilizopo ili kuchochea maendeleo ya nchi na kudumisha amani iliyopo.

Naibu Katibu Mkuu mstaafu wa Umoja wa Mataifa, Dkt. Asha-Rose Migiro, aliyasema hayo Dar es salaam jana wakati akizungumza na waandishi wa habari katika kilele cha siku ya amani duniani.

Alisema siku ya amani duniani ina umuhimu mkubwa kwa Watanzania kuhamasisha misingi ya uhuru, haki na uvumilivu.

Aliongeza kuwa, amani endelevu lazima ijengwe na maendeleo endelevu ili kuhamasisha shughuli za kiuchumi ambazo zinatunza mazingira na kuboresha ustawi wa jamii katika ngazi zote.

“Kama tutaendeleza kulinda aamani tuliyonayo, tutafanikiwa kuwa na maendeleo endelevu kwa maisha ya baadae,” alisema.

Siku ya amani duniani huadhimishwa Septemba 21 kila mwaka ambapo Tanzania ni mara ya kwanza kufanya maadhimisho hayo.

Kauli mbiu ya maadhimisho hayo mwaka huu inasema, “Amani endelevu kwa uendelevu wa maisha ya baadae”.

No comments:

Post a Comment