07 September 2012
Msanii Steve Nyerere arudisha fomu ya NEC
Na Mwandishi Wetu
MSANII nyota wa filamu nchini Steve Nyerere juzi alirudisha fomu na kufanyiwa usaili katika Ofisi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) , Wilaya ya Kinondoni ambapo anawania nafasi ya kungia katika Kikao Cha Halmashauri kuu ya Taifa ya chama hicho NEC.
Akizungumza mara baada ya kufanyiwa usaili Steve Nyerere alisema kwamba yuko tayari kwa kuwatumikia kichama na wasanii kwa ujumla, ikiwa ni njia moja wapo ya kuweza kutetea haki wasanii hasa wa filamu nchini.
“Huu ni mwanzo tu na na nimejitosa katika siasa ili niweze kuungana na wanachama wa chama ambacho nakipenda CCM na kuwakilisha wasanii kwa ujumla,” alisema Steve.
Aliongeza kwa kusema kuwa amethubutu kuingia katika siasa siyo kwa kushurutishwa bali amejikuta wito ukimtuma afanye hivyo, na kusema kwamba hata wasanii wenzake ambao wametangulia kama Khadija Kopa na John Komba imepa hamasa.
Aidha msanii huyo amepata baraka zote kutoka kwa Shirikisho la filamu nchini (TAFF),endapo atateuliwa Steve anatarajiwa kuwa mwakilishi wa kwanza wa wasanii wa filamu nchini kuweza kuingia katika vikao hivyo vikubwa vya chama hicho.
Wakati huohuo Steve Nyerere alisema kuwa, endapo atashindwa kupata nafasi ya ujumbe wa NEC, hatakata tamaa na atajipanga na kuangalia alikosea na siyo kukihama chama chake kwa kuwa ana mapenzi mema na chama hicho.
Nyerere kwa sasa anatamba na filamu ya ‘Mwalimu Nyerere’, aliyoizindua hivi karibuni katika kituo cha watoto yatima cha Maunga Center.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment