28 September 2012

Mkuu wa shule atamba kuinua vipaji vya michezo



Na Rabia Bakari

MKUU wa shule ya Sekondari ya wasichana ya Barbro Johannson ya jijini Dar es Saalam, Halima Kamote amesema kuwa licha ya kusimamia taaluma, lakini shule hiyo inasaidia kuinua vipaji mbalimbali vya michezo.

Akizungumza hivi karibuni, Kamote alisema kuwa kwa kiasi kikubwa wanaibua vipaji na kuvikuza ili wanafunzi hao watakapomaliza masomo wakatumikie vipaji vyao kama ajira.

"Tunaangalia, kama mtu ana kipaji cha kuwa mwanamitindo, mwimbaji, mwigizaji, na hata mbunifu kwa masuala ya sayansi nakadhalika, tunakuza kipaji hicho, na ndio kazi yetu kama shule,"alisema Kamote.

Aliongeza kuwa wao kama shule wanaamini kuwa vipaji ni ajira, hivyo kukuza vipaji vya wanafunzi vinasaidia kwenda kupambana katika soko la ajira baada ya wao kumaliza elimu yao hapo baadaye.

"Kwa sasa huwezi kusoma halafu ukawaza ukitoka hapo ukaajiriwe, fursa za ajira ni chache, hivyo ni muhimu kuweka wigo mpana wa kuanza kujiajiri kwa kipawa ulichopewa na Mungu, hautayumba katika maisha,"alisema.

No comments:

Post a Comment