17 September 2012

Mechi za Simba, Yanga zaingiza sh. milioni 118



Na Zahoro Mlanzi

MECHI za ufunguzi wa Ligi Kuu Bara kwa miamba ya soka nchini, timu za Simba na Yanga ambazo zilikuwa katika viwanja tofauti Dar es Salaam na Mbeya, zimeingiza sh. 118,228,000.


Simba ambayo ndio mabingwa watetezi, walianza kampeni ya kutetea ubingwa huo kwa kuumana na African Lyon kwenye Uwanja wa Taifa ambapo mechi yao iliingiza sh. 67,793,000 huku Yanga iliyoumana na Prisons ya Mbeya kwenye Uwanja wa Sokoine iliingiza sh. 50,435,000.

Kwa mujibu wa taarifa iluyotolewa kwa vyombo vya habari Dar es Salaam jana na Ofisa Habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Boniface Wambura ilieleza kwamba mashabiki 11,505 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo ambapo viingilio vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000.

Alisema kutokana na mapato hayo kila timu ilipata sh. 14,603,263.47 wakati asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyokatwa ni sh. 10,341,305.08.

"Mgawo mwingine umekwenda kwa Msimamizi wa Kituo sh. 20,000, posho ya kamishna wa mechi sh. 114,000, Mwamuzi wa akiba sh. 70,000, vishina kwenye tiketi (attachments) sh. 345,150, maandalizi ya uwanja sh. 400,000 na Wachina sh. 2,000,000.

Alisema gharama za umeme ni sh. 300,000, ulinzi na usafi uwanjani sh. 2,350,000, Kamati ya Ligi sh. 4,867,754.49, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 2,920,652.69, uwanja sh. 4,867,754.49, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 1,947,101.86, gharama za mchezo sh. 4,867,754.49.

Wakati huohuo, Wambura alisema watazamaji 112 ndiyo waliokata tiketi kushuhudia mechi ya  JKT Ruvu na Ruvu Shooting iliyofanyika juzi Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.

Alisema mapato yaliyopatikana katika mechi hiyo ambapo viingilio vilikuwa sh. 3,000 na sh. 10,000 ni sh. 340,000 ambapo kila timu iliambulia sh. 29,465.87, asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) sh. 51,864.40, maandalizi ya uwanja sh. 100,000 na tiketi sh. 89,916.

Alisema Kamati ya Ligi sh. 9,821.95, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 5,893.17, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 3,928.78, gharama za mchezo sh. 9,821.95 na uwanja sh. 9,821.95.

No comments:

Post a Comment