14 September 2012
Muogeleaji Agness apania kufikisha rekodi ya Olimpiki
Na Amina Athumani
MUOGELEAJI Agnes Kimimba amepania kukamilisha sekunde 08:40 katika mashindano mbalimbali ya kimataifa ili kukamilisha muda wa viwango vya Olimpiki.
Akizungumza na gazeti hili Dar es Salaam jana, muogeleaji huyo alisema nia yake kubwa ni kuhakikisha anacheza michezo ya Olimpiki ya mwaka 2016 itakayofanyika nchini Brazil.
Alisema kwa kushirikiana na Klabu yake ya Tanzania Marine Swiming Club (TMSC) atahakikisha anapata mashindano mengi ya ndani na nje ya nchi yatakayomuwezesha kuboresha muda wake.
Alisema muda wake wa kawaida ambao anautumia kwenye mashindano mbalimbali ni sekunde 35:20, hivyo ataupunguza na kufikia sekunde 28:00 muda ambao ndio wa kufuzu Olimpiki.
Muogeleaji huyo anashindana katika staili ya butterfly mita 50 ambapo kama atafuzu viwango vya Olimpiki itakuwa ni mtanzania wa kwanza kuwa na mwakilishi wa michezo ya Olimpiki kwa staili hiyo.
Waogeleaji wote wa Tanzania waliowahi kucheza michezo ya Olimpiki akiwemo Magdalena Mushi na Amaar Gadiyali wanashiriki umbali wa mita 50 staili huru (Free sty).
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment