05 September 2012

Kiiza, Okwi wampasua kichwa kocha Uganda



Na Mwandishi Wetu

KOCHA Mkuu wa timu ya Taifa ya Uganda 'The acranes', Bobby Williamson hajui amuanzishe mshambuliaji gani kati ya
Hamis Kiiza , Emmanuel Okwi na Godfrey Ssentongo katika mchezo wa Jumamosi dhidi ya Zambia wa kuwania kufuzu kucheza fainali za Mataifa ya Afrika mwakani.

Mchezo huo unatarajiwa kupigwa kwenye Uwanja wa Levy Mwanawasa, ambapo timu hiyo inatarajia kutua mjini Ndola nchini humo kesho.

Kwa mujibu wa gazeti la Daily Monitor la Uganda, kutokana na uwezo wa wachezaji hao inampa wakati mgumu kocha huyo raia wa Scotland, kujua nani ataongoza mashambulizi dhidi ya Zambia.

"Napata wakati mgumu mpaka sasa kuamua, lakini itanilazimu kuwachezesha washambuliaji wote watatu kwani sina shaka katika kuamua hivyo.

"Washambuliaji hao wanaweza, wanafunga mabao na kama nilivyosema watacheza wote, ingawa si lazima ila nitaamua kulingana na mechi husika Okwi, napenda aanze lakini kiwango kimekuwa chakupanda na kushuka tangu aende kufanya majaribio Austria na hakucheza mechi nyingi za ushindani.

Alisema Ssentongo ameonesha kiwango kizuri katika michuano ya Kombe la Kagame na Kiiza, pia ameonesha kiwango cha juu katika michuano hiyo kwa kufunga mabao sita.

Akimzungumzia zaidi Ssentongo, alisema ni mshambuliaji anayejituma na kuwasumbua mabeki na anakaa na mpira muda mwingi na hata akipoteza huangaika kuutafuta.

Aliongeza katika kikosi chake watakosekana wachezaji Brian Umony anayecheza soka la kulipwa Vietnam na Geoffrey Massa, anayecheza katika Afrika za Kaskazini kutokana na kuwa majeruhi, kitu ambacho kimemfanya aumize kichwa zaidi.

Timu hiyo inafanya mazoezi katika Uwanja wa Namboole, ikiwa na wachezaji 17 huku kocha huyo akiwa na matumaini ya kuibuka na ushindi kutokana na silaha alizonazo, wakati itakapowavaa mabingwa hao wa Afrika.

1 comment:

  1. 8 Nayajua matendo yako. Tazama, nimekupa mlango uliofunguliwa mbele yako, ambao hapana awezaye kuufunga, kwa kuwa unazo nguvu kidogo, nawe umelitunza neno langu, wala hukulikana jina langu.
    9 Tazama, nakupa walio wa sinagogi la Shetani, wasemao kwamba ni Wayahudi, nao sio, bali wasema uongo. Tazama, nitawafanya waje kusujudu mbele ya miguu yako, na kujua ya kuwa nimekupenda.
    10 Kwa kuwa umelishika neno la subira yangu, mimi nami nitakulinda, utoke katika saa ya kuharibiwa iliyo tayari kuujilia ulimwengu wote, kuwajaribu wakaao juu ya nchi.
    11 Naja upesi. Shika sana ulicho nacho, asije mtu akaitwaa taji yako.
    12 Yeye ashindaye, nitamfanya kuwa nguzo katika hekalu la Mungu wangu, wala hatatoka humo tena kabisa, nami nitaandika juu yake jina la Mungu wangu, na jina la mji wa Mungu wangu, huo Yerusalemu mpya, ushukao kutoka mbinguni kwa Mungu wangu, na jina langu mwenyewe, lile jipya.
    13 Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa.
    14 Na kwa malaika wa kanisa lililoko Laodikia andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye Amina, Shahidi aliye mwaminifu na wa kweli, mwanzo wa kuumba kwa Mungu.
    15 Nayajua matendo yako, ya kuwa hu baridi wala hu moto; ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au moto.
    16 Basi, kwa sababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto, nitakutapika utoke katika kinywa changu.
    17 Kwa kuwa wasema, Mimi ni tajiri, nimejitajirisha, wala sina haja ya kitu; nawe hujui ya kuwa wewe u mnyonge, na mwenye mashaka, na maskini, na kipofu, na uchi.
    18 Nakupa shauri, ununue kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto, upate kuwa tajiri, na mavazi meupe upate kuvaa, aibu ya uchi wako isionekane, na dawa ya macho ya kujipaka macho yako, upate kuona.
    19 Wote niwapendao mimi nawakemea, na kuwarudi; basi uwe na bidii, ukatubu.
    20 Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami.
    21 Yeye ashindaye, nitampa kuketi pamoja nami katika kiti changu cha enzi, kama mimi nilivyoshinda nikaketi pamoja na Baba yangu katika kiti chake cha enzi.
    22 Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa.
    Ufunuo3

    ReplyDelete