28 September 2012

Katibu BAKWATA asomewa shtaka la udanganyifu



Na Daud Magesa, Mwanza

KATIBU wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA), Wilaya ya Nyamagana, mkoani Mwanza, Bw. Hussein Mambosasa, jana imemsomea mashitaka ya kughushi na kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoani hapa.


Mshitakiwa ambaye anatetewa na wakili Bw. Anthony Nasimire,
alisomewa mashitaka hayo na Mwendesha Mashitaka wakili wa Serikali Bw. Sehewa Mamti.

mbele ya Hakimu Mkazi, Bw. Emmanuel Njuu, ilidaiwa mshtakiwa alitenda kosa hilo Oktoba 30 mwaka 1986.

Bw. Mamti aliiambia mahkama hiyo kuwa, mshitakiwa bila halali yoyote akijua ni kinyume cha sheria, alighushi maandishi na kuuza nyumba mali ya marehemu Mrisho Bakari na kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Alidai nyumba hiyo iliuzwa kwa sh. 200,000, baada ya mshtakiwa  kughushi maandishi kinyume na kifungu cha 302 cha kanuni na sheria ya makosa ya adhabu, sura ya 16 ambayo ilifanyiwa marekebisho mwaka 2002.

Baada ya kusomewa shitaka hilo, mshitakiwa alikana kutenda kosa hilo na yuko nje kwa dhamana. Kesi hiyo ya jinai namba 526 iliahirishwa hadi Oktoba 24 mwaka huu.


Shauri hilo lilifunguliwa mahakamani hapo Agosti 15 mwaka huu na Bw. Bakari Mrisho ambaye ni mtoto wa marehemu akipinga kuuzwa kwa nyumba ya marehemu baba yake bila kushirikishwa.

Mshtakiwa anadaiwa kushirikiana na Bw. Saad Ally na Bw. Ramadhan Samamba kuuza nyumba hiyo baada ya kujifanya ndugu wa marehemu Mrisho. Nyumba hiyo ilinunuliwa na Bw. Suleman Salim Mbaraka.

No comments:

Post a Comment