17 September 2012

Itambue siri ya kuishi miaka mingi


Na Godfrida Jola na Mashirika

TAFITI mbalimbali zimebaini kuwa, watu wanaotembea mara kwa mara huishi muda mrefu, wana uzito unaofaa, hawana shinikizo la damu na wanaishi maisha ya raha kuliko wanaotumia magari kwa muda mrefu.

Tafiti 26 zilizofanywa na wanasayansi mbalimbali zimebaini kuwa unapotembea huku ukiwa na viatu vifupi hatua 2100 kwa siku husaidia mwili kuimarika na kushambualia magonjwa.

FAIDA ZA KUTEMBEA

Huongeza umri wa kuishi. Utafiti uliofanywa mwaka 2011 umebaini kuwa kutembea zaidi ya saa moja kwa siku huongeza umri wa kuishi kwa kiasi kikubwa. Utafiti uliangalia washiriki 27,738 wa umri kati ya miaka 40 na 79 kwa miaka 13 na kubaini kuwa gharama za matibabu hazikuongezeka licha ya umri walioishi.

"Ongezeko la gharama za matibabu wanaotembea kwa muda fulani wafikiapo uzee kwani huitaji mahitaji malumu kwa fedha nyingi za dawa, kutembea humaliza ugonjwa wa kisukari," utafiti umebaini.

Unapotembea kwa nusu saa katika siku moja unajikinga na kisukari, utafiti wa mwaka 2002 uliangalia watu wenye uzito mkubwa na kubaini kuwa wapo katika hatari ya kupata magonjwa ya shinikizo la damu na kisukari.

Utafiti uliofanywa mwaka 2007, umebaini kuwa, kama una ugonjwa wa sukari kutembea ni njia ya kukusaidia kumaliza tatizo hilo. Unapotembea mara nyingi inakupunguzia hatari ya kupoteza maisha.

Kutembea maili sita  hadi nane kwa wiki husaidia kuongeza uwezo wa kuweka kumbukumbu na kupunguza mateso ya uzeeni ya kupoteza kumbukumbu, hii imebainika na utafiti uliofanyika kwa watu 299 katika kipindi cha miaka 9.

Aidha, kutembea maili tano kwa wiki inaweza kutoa ulinzi katika ubongo usishambuliwe na ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu, wale ambao tayari wanaosumbuliwa na ugonjwa huo wanapotembea husaidia kupungua na kurudi katika hali ya kawaida.

KUTEMBEA HUTIBU SHINIKIZO LA DAMU

Shinikizo la damu linaweza kuisha unapotembea kwa dakika 30 kwa siku, mara tano kwa wiki hata usipozimaliza ukatembea asubuhi mchana na jioni hadi kufikia dakika hizo unajitibu.

Shinikizo la damu ndicho chanzo kikubwa cha ulemavu
na vifo vya mapema nchini Uingereza, kupitia kiharusi,
mshtuko wa moyo na maradhi ya moyo.

Mmoja kati ya watu wazima watatu nchini Uingereza ana shinikizo la damu, na kila siku, watu 350 hukumbwa na kiharusi kinachoweza kuzuiwa unasababishwa na hali hii.

Shirika la Afya Duniani, WHO, limesema watu wengi zaidi katika maeneo yote duniani wako katika hatari ya kupata ugonjwa wa kupooza, maradhi ya moyo na saratani.

Takwimu zake za mwaka 2012 kutoka nchi zote wanachama 194, WHO imesema hali kama za shinikizo la damu na unene wa kupita kiasi vinaongezeka kutokana na watu kula vyakula vingi vya mafuta, sukari na chumvi na kushindwa kufanya mazoezi.

Kila mtu mzima mmoja kati ya watatu duniani ana ongezeko la shinikizo la damu, hali ambayo inasababisha karibu nusu ya vifo vyote vitokanavyo na kiharusi, na maradhi ya moyo.

Takwimu hizi ni kutokana na ripoti mpya ya shirika la afya dniani (WHO) ambayo pia inasema mtu mzima mmoja kati ya kumi duniani ana ugonjwa wa kisukari.

Hata hivyo nchi za Afrika zilizo kusini mwa Jangwa la Sahara zaidi ya asilimia 40 hadi 50 ya watu wazima wanakadiriwa kuwa na shinikizo la damu.

Unapotembea husaidia moyo wako kuisafirisha damu mwilini kirahisi na kuupa mwili nguvu na hewa aina ya oxygen ambayo mwili unahitaji. Damu inaposogea, huwa inajisukuma kwenye kingo za mishipa ya damu. Nguvu ya msukumo huu ndio msukumo wa damu.

Pia kutembea ni tiba ya mifupa, unapopishanisha miguu katika maili moja unaimarisha mifupa yako na kukuepusha kupata matatizo ya miguu na kupooza pia.

Ikiwa msukumo wa damu yako uko juu, basi unaufanyisha moyo na mishipa yako kazi nyingi. Kwa muda, hii kazi nyingi huenda ikafanya viungo vya mwili kuharibika, na kukuweka katika hatari ya matatizo ya kiafya.

Shinikizo la damu mwilini linaweza pia kusababisha maradhi ya
moyo na figo pia, na linahusiana na aina fulani za kichaa.

Unapoendelea kuzeeka, athari za mitindo ya maisha isiyokuwa ya kuendeleza afya bora zinaweza kurundikana na kuongeza viwango vya msukumo wa damu yako.

Unapotembea kwa dakika 30 mara tano kwa wiki, unaweza kuufanya moyo wako kuwa na afya nzuri, na kupunguza msukumo wa damu yako.

Utafiti umebaini kuwa huchukua zaidi ya miaka saba kwa mtu aliyepooza katika umri mkubwa kurudi katika hali yake.

Ukitembea kwa takribani maili 12.5 kwa wiki ama zaidi unapunguza hatari ya kupata ugonjwa wa kupooza. Utafiti uliofanywa kwa watu 11,000 waliokuwa na tabia ya kutembea katika umri wa miaka 58 ulibaini kutokuwa na magonjwa ya aina hii.

Ikiwa una msongo wa mawazo kutembea ni njia rahisi ya kumaliza tatizo hilo na kuondosha hatari ya kupata ugonjwa wa shinikizo la damu ambalo husababishwa na msongo wa mawazo.

Tafiti zimebaini kuwa kutembea kwa dakika 20 kwa siku unaongeza miaka 7 ya kuishi kuliko hata kutumia lishe bora.

Kutembea pia husaidia kumaliza tatizo la kukosa usingizi, unapotembea kwa dakika 45 kula asubuhi kwa muda wa siku tano tatizo hilo litamalizika.

"Tatizo la kukosa usingizi huwapata wanawake wenye umri wa miaka 50-74, wanashauriwa kutembea ili kuondokana na tatizo hilo,".

Utafiti uliofanywa kwa zaidi ya wanawake 72,000 wenye umri wa miaka 40-65, waliokuwa na matatizo ya shinikizo la damu walishauriwa kutembea na kupunguza vifo kwa asilimia 30 hadi 40.

Nchini Marekani zaidi ya wanawake wenye umri wa miaka kati ya 40-65 kutokana na shinikizo la damu huku wanaume wenye umri wa miaka 73-93 wakishambuliwa na magonjwa hayo.

Watu hupoteza maisha katika umri mdogo siku hizi kutokana na shinikizo la damu na kiharusi kutokana na kukosa mazoezi ya mwili.

Nfano unatoka ofisini unaingia katika gari hadi nyumbani ukifika unakula na kulala ni wazi unajitakia magonjwa kwani mwili haujatoka jasho ili kupunguza sumu uliyoingiza kupitia chakula na hewa uliyovuta kwa siku.

Kutembea husaidia kupunguza uzito, kuondoa nyama zembe mwilini, kupunguza mafuta (fat), na kukufanya uwe mwepesi wa kufikiri.

Kutembea hakuna ugumu wala gharama, unaweza kupanga muda wako na ukaweza.

Tuache tamaduni za kwenda na wakati ili tuishi kama walivyoishi zamani kwakuwa hakukuwa magari walitembea umali mrefu kufuata huduma muhimu za jamii.No comments:

Post a Comment