28 September 2012
Dj kutoka Kenya Nijo 'kukamua' San Siro leo
Na Amina Athumani
WASANII wa filamu na wanamuziki mbalimbali nchini leo watajumuika pamoja katika shoo ya muziki itakayoendeshwa na Dj Nijo kutoka nchini Kenya kwa kushirikiana na ma Dj wa Tanzania.
Akizungumza Dar es Salaam jana, mara baada ya kutua jijini Dar es Salaam akitikea nchini Uganda alipokuwa akiendesha shoo kama hiyo, Dj Nijo alisema huo ni mpango wa kuzunguka nchi za Ukanda wa Afrika Mashariki kuungana na ma Dj wa nchi hizo katika kubadilishana burudani.
Alisema alikuwa nchini Uganda kwa shoo kama ambayo ataiendesha Tanzania kwa kushirikiana na Ma Dj wa hapa nchini kama Dj Mkali, H'cue, Peter Moe na Dj Celvin.
Akizungumzia onesho hilo Dj H'Cue alisema pamoja na mashabiki wa muziki pia watakuwepo wacheza filamu maarufu nchini kama JB, Ray na Aunt Ezekiel ambao wataungana na wasanii wengine katika onesho hilo.
Alisema shoo hiyo itafanyika katika klabu ya San Siro ambayo imepewa jina la usiku wa fleva na kwamba imeandaliwa na kudhaminiwa na kampuni ya ving'amuzi ya Zuku.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment