28 September 2012
CHANETA yataja timu za Muungano
Na Amina Athumani
CHAMA cha Netiboli Tanzania Bara (CHANETA), kimeteuwa timu nne zitakazoshiriki Ligi ya Muungano ambayo itashirikisha pia timu nne za Zanzibar.
Timu hizo ni Filbert Bayi, JKT Mbweni, Jeshi Star na Magereza Morogoro, ambazo zimekata tiketi hiyo kupitia mashindano ya Ligi Daraja la Kwanza yaliyomalizika hivi karibuni mkoani Mbeya.
Akizungumza na gazeti hili Mwenyekiti wa CHANETA, Anna Bayi alisema timu za Zanzibar zitatokana na ligi ya Zanzibar ya mchezo huo, ambazo nazo timu nne za juu zitapata nafasi ya kushiriki mashindano hayo.
Alisema baada ya kumalizika kwa ligi ya Tanzania bara timu zote zilizopata nafasi ya kushiriki ligi ya Muungano zitaendelea na maandalizi hadi hapo tarehe ya ligi itakapotangazwa.
Alisema timu zote nne zina kiwango kikubwa cha mashindano hivyo, anaimani ligi ya Muungano itakuwa na ushindani mkubwa kutokana na baadhi ya timu kuwa na wachezaji wengi chipukizi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment