14 September 2012

BFT yaunda kamati kusimamia mashindano Taifa


Na Mwali Ibrahim

SHIRIKISHO la Ngumi za Ridhaa Tanzania (BFT), limeunda kamati itakayosimamia mashindano ya Taifa yanayotarajia kufanyika Septemba 17, mwaka huu katika Uwanja wa Ndani wa Taifa ili kuhakikisha mashindano hayo yanafanyika kwa kiwango cha Kitaifa.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa BFT, Makore Mashaga alisema  kamati hiyo imeundwa kwa kuwajumuisha wataalamu wa ufundi kutoka  kamati za BFT, mabondia wa zamani na wataalamu wa mipango na fedha kutoka katika taasisi na mashirika ambayo yamekuwa mstari wa mbele kusaidia kwa vitendo shughuli na matukio mbalimbali ya BFT.

Aliwataja wajumbe walioteuliwa kuunda kamati hiyo kuwa ni Andrew Kweyeyana ambaye ndiye Mwenyekiti wa Kamati, Willy Issangura, Juma Suleiman, Remy Ngabo na Mohamed Kasilamatwi.

Wengine ni Said Omari, Antony Mwang’onda, Joel Magori, Charles Jilaba na Undule Mwampulo ambao wote hao waliweza kusaidia kwa namna moja au nyingine kwa bondia pekee hapa nchini, Selemani Kidunda kuweza kufuzu  mashindano ya Olimpiki yaliyofanyika hivi karibuni London, Uingereza.

"Jukumu walilopewa ni kuhakikisha mashindano yanafanyika kwa kufuata taratibu zote za chama cha Ngumi cha Dunia (AIBA) na kuhakikisha fedha za kuendesha mashindano zinapatikana na majukumu ya kamati hiyo yatamalizika baada ya kumalizika kwa mashindano hayo.

No comments:

Post a Comment