14 September 2012
TFF yapitisha kanuni ligi za mkoa, wilaya
Na Amina Athumani
KAMATI ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), imepitisha marekebisho ya kanuni kwa ajili ya Ligi ya Mkoa na Ligi ya Wilaya.
Kamati hiyo imepitisha marekebisho hayo katika kikao kilichofanyika juzi jijini Dar es Salaam.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura alisema marekebisho hayo yametokana na mabadiliko ya mfumo wa mashindano uliofuata Ligi ya Taifa.
Alisema hivi sasa kutakuwa na Ligi Kuu, Ligi Daraja la Kwanza, Ligi ya Mkoa na Ligi ya Wilaya.
Wambura alisema kutokana na marekebisho hayo ya kanuni ya Ligi ya Wilaya itaendeshwa na Vyama vya Mpira wa Miguu vya Wilaya (DFAs) na Ligi ya Mkoa itaendeshwa na Vyama vya Mpira wa Miguu vya Mikoa (RFAs).
Alisema mechi za mchujo kutafuta timu zitakazopanda kwenda Ligi ya Mkoa zitaendeshwa na RFAs wakati za kupanda Ligi Daraja la Kwanza zitakazohusisha mabingwa wa mikoa zitasimamiwa na TFF.
Wambura alisema ligi za madaraja yote zitachezwa mwaka mzima kwa mtindo wa nyumbani na ugenini.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment