27 August 2012

Watoto wa kike watakiwa kujitambua



Na Victor Mkumbo

WANAWAKE wenye umri chini ya miaka 18, wametakiwa kujitambua ili kuweza kufikia malengo waliyojiwekea.

Akizungumza katika Semina ya waschana wenye umri wa kuanzia miaka 11 mpaka 18 juzi, Mkurugenzi wa Shirika la TWA, Irene Kiwia alisema kuwa vijana wanatakiwa kujitambua ili kuweza kufikia malengo.


Alisema kuwa wameamua kuanzisha Semina hiyo kwa ajili ya kutoa elimu kwa Wanawake ambao wana umri mdogo kwa ajili ya kujikinga na majanga mbalimbali.

Alisema kuwa semina hiyo elekezi ni kwa ajili ya kuwajengea uwezo watoto wa kike ili waweze kujitambua na kujua nafasi zao katika familia na jamii inayowazunguka.

Alisema kuwa katika semina hiyo pia  wameweza kuwajengea ujasiri wa kutambua haki zao za msingi.

Bi. Irene alisema kuwa pia watoto wa kike wanatakiwa kujua athari za magongwa yanayotokana na ngono ikiwa ni pamoja na maambukizi ya Ukumwi.

Alisema kuwa kumekuwa na watoto wengi wa kike ambao wanaacha shule kutokana na matatizo mbalimbali ikiwa ni pamoja na mimba za utotoni ambapo wameamua kuanzisha kampeni ya Kinara Ni Mimi Jasiri ambayo pia wanatarajia kuipeleka katika mikoa mbalimbali.

Alisema kuwa malengo yao ni kuweza kutoa elimu kwa watoto wa kike katika mikoa ya Tanzania bara pamoja na Visiwani ili kufikia malengo.

“Dhumuni letu kubwa ni kuwatengeneza vinara ili waweze kuwa na programu endelevu ambayo inaweza kuwasaidia katika maisha yao ya baadaye na kufikia malengo” alisema Bi Irene.

No comments:

Post a Comment