21 August 2012
Utaratibu wa kukimbiza Mwenge ubadirike'
Na Jovither Kaijage, Ukerewe
BAADHI ya wakazi wa Wilaya ya Ukerewe, mkoani Mwanza, wameishauri Serikali kuachana na utaratibu wa kukimbiza Mwenge wa Uhuru kila mwaka ili kuepusha gharama ambazo si za lazima.
Ushauli huo umetolewa jana kwa nyakati tofauti baada ya uongozi wa Mkoa huo, kuupokea Mwenge wa Uhuru na kuanza kuukimbiza katika Wilaya saba mkoani hapa.
Walisema umefika wakati wa Serikali kuangalia upya utaratibu wa kuukimbiza mwenge huo nchi nzima kwa sababu manufaa yake ni madogo ukilinganisha na gharama zinazotumika kuukimbiza.
Mmoja wa wakazi hao, Ainex Kagambirwe, alisema inasikitisha kuona fedha nyingi za walipa kodi zinatumika kukimbiza mwenye huo wakati Watanzania wengi wanakosa huduma muhimu kama matibabu na elimu bora.
“Fedha na rasilimali zinazotumika kukimbiza Mwenge wa Uhuru kila mwaka ni vyema zikatumika kuboresha huduma za jamii kama ununuzi wa madawati, vifaa vya shule, dawa na vifaa tiba.
Alisema kama kuna ulazima wa kuukimbiza kila mwaka, Serikali itenge fedha za kazi hiyo badala ya kutegemea michango ya wananchi ambayo hivi sasa imekuwa kero kwao.
“Suala la kuenzi utamaduni wa Taifa ni lazima lakini kuendelea kutumia gharama kubwa kwa jambo hili wakati Watanzania wengi hawana huduma muhimu sio sahihi hivyo upo umuhimu wa kukimbiza mwenge mara moja kila baada ya miaka mitano.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
nimeshuhudia zoezi la kukimbiza mwenge huko tangu miaka ya sitini kwa kweli kulikuwa na msisimko mkubwa sana,na watu waliona kuwa mwenge ni alama halisi ya utaifa.
ReplyDeletelakini siku hizi mwenge umepoteza hadhi yake kwa kiwango kikubwa kwani kwanza haufiki sehemu nyingi katika wilaya aidha kutokana na UKIMWI watu wamekuwa wakipata maambukizi kutokana na mikesha.Zaidi ya hapo ile kazi ya kuchochea maendeleo tena haipo ninaungana na pendekezo la kuwa mwenge ukimbizwe angala kila baada ya miaka mitatu au mitano na maandalizi yawe yakutosha kwa miradi ya maendneleo na watu pia.