21 August 2012
Ulimboka aibukia kanisani Ubungo *Atoa sadaka maalumu, awashukuru Watanzania *Adai unyama aliofanyiwa anamuachia Mungu
Stella Aron na Rehema Maigala
HATIMAYE Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari nchini, Dkt.Steven Ulimboka, ameibuka na kusema kitendo cha kinyama alichofanyiwa na watu waliomteka anamuachia Mungu.
Dkt.Ulimboka aliyasema hayo Dar es Salaam juzi alipokwenda kutoa sadaka ya shukrani na familia yake kwenye Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Ubungo.
Katika ibada hiyo, Dkt.Ulimboka ambaye pia alisindikizwa na ndugu zake wa karibu, alimshukuru Mungu kwa kumpigania maisha yake na kurudi salama, madaktari wenzake na Watanzania wote kwa maombi yao ambayo yamemwezesha apone haraka.
Kabla ya kutoa sadaka maalumu, Dkt. Ulimboka aliomba kusomewa kitabu cha Zaburi 124 isemayo; “Kama si Bwana aliyekuwa pamoja nasi, Israel na aseme sasa, kama si Bwana aliyekuwa pamoja nasi, wanadamu walipotushambulia, wangalitumeza hai”
“Hasira yao ilipowaka juu yetu, papo hapo maji yangalitugharikisha, mto ungalipita juu ya roho zetu, papo hapo yangalipita juu ya nafasi zetu yafurikayo”
“Na ahimidiwe Bwana, asiyetutoa kuwa mawindo kwa meno yao, nafasi yetu imeokoka kama ndege katika mtego wa wawindaji, mtego umevunjika nasi tumeokoka, msaada wetu u katika jina la Bwana aliyezifanya mbingu na nchi”
Baada ya kusomwa ujumbe huo, Mchungaji wa kanisa hilo Godlizen Nkya Mkaya, alimwongezea sura nyingine ya Zaburi 44, kuanzia mstari wa kwanza hadi wa saba na kusomwa kanisani hapo.
Baadhi ya maneno ya sura hiyo yalisema; “Ee Mungu tumesikia kwa masikio yetu, Baba zetu wametuambia matendo uliyoyatenda siku za kale, wewe kwa mkono wako uliwafukuza mataifa ukawakalisha wao”
“Maana si kwa mkono wao walivyoimiliki nchi wala si mkono wao uliowaokoa, bali mkono wako wa kuume, Mungu wewe ndiwe mfalme wangu, uagize mambo ya wokovu kwa Yakobo”
“Kwa nguvu zako tutawaangusha watesi wetu, kwa nguvu zako tutawakanyaga watupingao, maana sitautumaini upinde wangu wala upanga wangu hautaniokoa bali wewe ndiye uliyetuokoa na watesi wenu na watuchukiao umewaaibisha,”
Baada ya ujumbe huo, Dkt. Ulimboka alisema yeye anamshukuru Mungu kwa kumponya na hana neno lingine zaidi ya hilo.
“Sina cha kusema kwa jinsi ambavyo Mungu amenitendea wema wake hivyo yote namuachia Bwana,” alisema Dkt.Ulimboka ambaye hakupenda kuzungumzia zaidi tukio lililomkuta.
Katika ibada hiyo, pia kulikuwa na uzinduzi wa CD ya kwaya ya Uinjilisti Kanani ambapo Dkt.Ulimboka, alinunua CD hiyo yenye nyimbo 10 kwa sh. 300,000.
Mwinjilisti wa kanisa hilo, Bw.Lenard Paulo, alisema CD hiyo ni ya tisa kutolewa na kwaya hiyo na wako mbioni kurekodi video yake.
“Kitendo alichofanyiwa Dkt.Ulimboka ambaye ni muumini wetu ni cha miujiza ya Mungu, Mwacheni Mungu aitwe Mungu tu...sina la kuzungumza zaidi ya hapa,” alisema Bw.Paulo.
Kutekwa kwa Dkt.Ulimboka, kuteswa na kutupwa katika msitu wa Mabwepande, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam, kumegusa hisia za makundi mbalimbali ya watu wakiwemo wanaharakati, madaktari wenzake na Watanzania kwa ujumla.
Kutokana na majeraha aliyokuwa nayo kutokana na kipigo, Dkt. Ulimboka alikimbizwa nchini Afrika Kusini kwa matibabu na baada ya kurejea nchini, Katibu wa Jumuiya ya Madaktari, Dkt.Edwin Chitage, alizungumza na vyombo vya habari na kusema wanaandaa utaratibu maalumu wa mwenzao kuzungumzia tukio zima.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
sawa dr ulimboka na sisi tuliopoteza wapendwa wetu kwa sababu ya mgomo ulioratibu wewe tunamuachia mungu. na sala zetu amezisikia na kaanza kukupa mfano wa itakavyo kua siku ukirudi kwake
ReplyDeleteHATUSHANGAI HATA SHETANI ALIMWAMBIA YESU IMEANDIKWA TUMIA MALAIKA WAKE MIKONONI MWAKE ILI ASIUKWAE MGUU WAKE KWA MSINGI HUO SHETANI ANAIFAHAMU SANA BIBILIA NAONA ANAWEWESEKA KUTOKANA NA MIZIMU YA WATU WALIOLAZIMISHWA KUFA KUTOKANA NA MGOMO HARAMU
ReplyDeletewatanzania tuache siasa katika uhai wa watu, dr. alikuwa anapigania vitendea kazi kwa madaktari ili uhai wa watanazania wengi uwe salama sasa nashangaa hawa mambumbumbu wasiojua maana hata ya ule mgomo wanafurahia yaliyomkuta Ulimboka, kumbukeni yeye alikua kiongozi sio wa mgomo ila wa kundi kubwa la madaktari ambao ndio waliotaka mgomo uwepo... watanzania tubadilike...
ReplyDeleteWewe ndiyo mbumbumbu toka lini vifaa vikapatikana kwa migomo tena haramu,utawala ulishasema utaviagiza kwa awamu hata maslahi yao yatashughulikiwa kwa awamu,mgomo wa nini tena wa kusababisha vifo tena vingi kwa wagonjwa masikini watanzania eti unawapigania wapewe vifaa tiba,hivyo vifaa vya nini tena wakati wagonjwa walishakufa,ashukuru mungu amepona hiyo ni miujiza ya mungu ili ajutie alichokuwa akikipigania na ajue kuwa siyo wote waliokuwa wanafurahia vitendo vyake viovu kwa maisha ya wanadamu kama yeye,nashukuru amekiri kuwa anafunga domo lake chafu tena aliweke kufuli kabisa wengine bado tuna hasira nae tena mbaya kabisa,hawezi kusababisha wapendwa wetu wapoteze maisha na yeye aendelee kuonja hewa ya bure ya mungu na kuendelea na uovu,udaktari ni wito kama hana wito atafute kazi nyingine isiyokuwa na bughudha afanye asituletee hizo zake mbovumbovu.
Deletehao wanaocoment bila kufikiri ni bora wakauze karanga mitaani kuliko kucoment mambo yanayoweza kumpa hasira ulimboka mpaka akaamua kufanya mambo mengine mabaya yanayoweza kuliingiza taifa katika mgogoro mwingine unaoweza kuleta maafa makubwa zadi... acheni unafki na mawazo mgando yasiyoyakimaendeleo na ya kipuuzi, badilisheni mitazamo ya akilili zenu hizo zilizogandamana kama matope...acheni ushabiki wa kimasikini
ReplyDeletewewe mbwa ndio mnafiki na muoga,alete tu hayo maafa kwani ameshaleta makubwa hivyo hatushangai na mengine. maafa anayapata baba,mama yako na jamaa zako malofa lakini mwenye pesa anaenda private hospital. kwani wameisha ambiwa wanachokitaka hakiwezekani kuna sababu ya kungangania hapo hospital za serikali si waende huko kwenye vioski vyao? au huko hamna nafasi ya kuiba dawa,kutumia vifaa vya bure kwa maslahi yao,au kumuomba rushwa mgonjwa? acha kunena hovyo.
Deletehaiwezekani kumtetea msababisha vifo eti anatetea uhai. kwani hakuna utaratibu mwingine wa kudai maslahi na kutetea uhai zaidi mgomo ambao unawaumiza na kuwauwa watu wa kawaida na sio hao watawala acheni ushabiki ktk maisha ya mwanadamu
ReplyDeleteWAPUUZI HAO ACHANA NAO. HILO KANISA ALILOKWENDA LABDA LA MASHETANI NDIO MAANA WAKAMPOKEA. HUYU HAKUTII AMRI ZA MUNGU KAMA VILE ANAVYOKATALIWA MTU KUZIKWA ASIYEHUDHURIA MISA. HIVYO HATUSHANGAI NA HILO KANISA. NI LA MASHETANI
DeleteNdugu zangu SHETANI au MTU MBAYA hafi haraka angalieni stiri za watu makatili na watu wema maisha yao yanakuwaje. Mtu mwema hadumu lakini HUYO SHETANI ULIMBOKA ATADUMU MUDA MREFU. IBILISI ALIKUBALI KUINGIA MOTONI LAKINI NIA YAKE YA KUPOTEZA WATU HAKUMKUBALIA MUNGU. SASA HUYU ATI ANAMUACHIA MUNGU NA SISI TULIOTAABIKA NA WALIOKUFA KUTOKANA NA MGOMO ALIOUVALIA NJUGA TUNAMUOMBA MUNGU HUYOHUYO AKUPE ADHABU NYINGINE. HUO NI MWANZO TU. MIMI NI MMOJA NILIOKUWA NAKUOMBEA MATESO MENGI ZAIDI LAKINI KAZI YA MUNGU HAINA MAKOSA. UMERUDI KUJA KUTESA WANANCHI KAMA VILE IBILISI ALIVYOKUBALI MOTO KWA KUPTEZA WATU. WALIOKUTESA NI HAOHAO CHADEMA WALIOKUTUMIA KWANI HATA MAELEZO YANAYOTOLEWA YANAKINZANA. CHEZA NA WANASIASA WA KIAFRIKA CHA MOTO UMEKIONA. NA SISI TULIMUACHIA MUNGU AKAKUBIP.
ReplyDeletePole sana Dr Ulimboka Mungu amekuponya karibu tena ili uendelee kulitumikia Taifa.
DeleteNdugu yetu anasema anamwachia Mungu kwa yote aliyofanyiwa , ni vizuri kusamehe kama neno linavyosema kisasi niachie mimi.
Lakini tukio hili pamoja na mengine yanayofanana na hayo naomba tujifunze kitu.
Kwanza mgomo ni kitu kibaya , kwa namna yoyote ile .
Mgomo unarudisha maendeleo ya taifa, unaleta athari nyingi madhara mengi ,kama tulivyoona kuwa wagojwa wengi walipoteza maisha kwa sababu ya mgomo huo, Aidha gharama za matibabau katika hospitali binafsi zilipanda hivyo kuathiri kwa namna moja au nyingine pato la mwananchi.
Lakini lazima hapa tuangalie kuwa ng;ombe au punda unaweza kumpeleka kwenye dibwi la maji kwa nia ya kumnywesha lakini asinywe hayo maji Wapo madaktari waliokuwa watiifu kwa kiapo chao na hawakushiriki kwenye mgomo huo na wakaendelea kufanya kazi.
Kama wote wasingemsikiliza Dr Ulimboka na kufuata kanuni na agano waliloagana na serikali kwenye ajira haya yote yasingetokea Aidha kwa upande mwingine serikali ilitakiwa kuchukua hatua za dharura kuanzia siku ya kwanza na kuwasimamisha kwa kwenda kinyume na kiapo chao na kutafuta madaktari mbadala toka jeshi au hata nje ya nchi wakati wanatafuta juu ya kutatua mgogoro wao au kuwapeleka mahakamani kama ilivyofanya kwa walimu
Kama nilivyosema mgomo ni kitu kibaya siyo muda mrefu tulishughudia kusimama kwa uchimbaji wa madini huko kanda ya ziwa kutokana na sheria mpya ya mafao ya uzeeni
Wiki iliyopita huko kwenye machimbo ya dhahabu Afrika kusini wachimbaji 34 walipigwa risasi kwa sababu waliandamana kudai kuongezewa marurupurupu,na hata baada ya vifo hivyo hilo bado halijawa suluhisho kwani waliobaki wameanza kwenda kazini lakini hawafanyi kazi.
Waajiri na waajiriwa inafika mahali kukaa pamoja na kuangalia swala la malipo na siyo kuvutia upande mmoja . Kwani hata neno la Mungu toka waraka wa Yakobo sura 5;3 -4 inasema:Dhahabu yenu na fedha yenu zimeingia kutu, na kutu yake itawashughudia, nayo itakula miili yenu kama moto. Mmejiwekea akiba katika siku za mwisho. Angalieni ujira wa wakulima waliovuna mashamba yenu, ninyi mliouzuia kwa hila ,unapiga kelele , na vilio vyao waliovuna vimeingia masikioni mwa Bwana wa Majeshi
Waajiriwa wengi wanaangalia pato la Taifa na jinsi watu wengine wanavyoishi hususani wanasiasa na kugundua kuwa mapato hayo hayagawanywi kwa haki ni hii huenda ndio chanzo cha migomo hiyo .
Ni wakati umefika tukarudi tulikotoka enzi ya utawala wa mwalimu Julius Nyerere aliyetumia pato la Taifa kwa ajili ya watanzania wote.
Mungu ibariki Tanzania
Naungana na wang'oa hoja na ni kweli huku jamaa aliratibu migomo uliosababisha wapenda wetu wengi kufariki. Dr ajutie kwanza na atubu kwa mwenyezi Mungu juu ya uharamia aliowafanyia watanzania. Hakuna mbumbumbu.hapa tafadhari.
Deletehuyo jamaa anayempinga ulimboka ni mbumbumbu kwa kuwa tanzania huwezi kupata haki bila mgomo au llenyewe lipo serikalini nini?
ReplyDeletePole Sana Dr.Steven Ulimboka, Wamekuzuia usiwataje waliokupiga nn?
ReplyDeleteWote tunaijua serikali yetu, mm sishangai wale wanao kuombea mabaya kwani hata katika maandiko imeandikwa "watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa". Wanaomponda DR. ULIMBOKA NI WAVUTA BANGI HIVYO VICHWA VYAO VIMEJAA MOSHI WA BANGI. Wajinga sana!
Eti serikali haina Fedha ya kununua vifaa vya hospitali!! wanaomponda Dr. Ulimboka waende hospitali za vijijini mjionee wenyewe KENGE nyie.
Kila wiki tunasikia ufisadi wa mabilioni hapa nchini au mnaomponda Dr. Ulimboka na CCM ni kitu kimoja,Ebu Fungukeni acheni UJUHA.
Huyu Dkt Ulimboka atueleze nini kilimtokea. mbona mpaka sasa hajasema kitu? Anachoogopa ni nini? mbona hakuogopa kusimamia au kuongoza mgomo wa madaktari. Nadhani kuna jambo anaficha hapa. isijekuwa ni Dili lake kuharibika ndio maana akapata kipigo. Asitudanganye kuwa anaiogopa serikali.Namwombea maisha mazuri yasiyo na matatizo lakini atueleze yaliyotokea ama sivyo stori zitatolewa nyingi kuhusu kilichomtokea (conspiracy theories.
ReplyDeleteKwanza jamaa zake walisema alikuwa akikata kinywaji leaders club ndipo aliopotekwa,baadaye hao hao jamaa zake wanasema aktekwa barabarani akiwasubiri waliompigia simu. huu ni mchezo wa kweli wa kuigiza. hivi wewe mwananchi huyu shetani Ulimboka katika hali kama ile aliweza kuwakimbia watekaji wake? huu mchezo mchafu wa siasa za Chadema kujipatia mamlaka kwa hali yoyote ile. Waliomteka ni Chadema na baadaye haohao wakamukota kumpeleka hospitali.
ReplyDeleteni vema ameona jinsi matibabu yanavyohitajika. mgomo si busara kabisa. kwanza yeye ananufaika na migomo kwa kuwa vijiwe vyake vinachanganya wakati wa mgomo. mbaya zaidi baadhi ya madaktari yawezekana wanatumia muda wa serikali kufanya kazi katika hospitali zake. yawezekana ni Mpango wa Mungu kuepusha kifo chake ili aweze kuaibika duniani-live
ReplyDeleteSerikali iliamua kuwasomesha madaktari bure si kwa kuwafanya kuwa wawe mungu watu. hawawezi kufanya kazi bila kushirikiana na wengine km wahandishi wanaowarahishia utendaji kwa kudesign vifaa mfano x-ray mc, robots, ecg mc nk, wahasibu.
fikiria marubani nao wangegoma kumpeleka Afrika kusini ingekuwaje?
Hawa madaktari sio huenda wanafanya katika vijiwe vyao wao huviita viosk. hii migomo yao ni sawa na mambo yaliokuwa yanafanyika Tanesco watu wanafanya makusudi umeme ukosekane halafu waanze kujaza matumbo yao,kwani sasa hivi imeongeza nini kwenye umeme zaidi ya uongozi. Hivyo wtanzania lazima tuwe makini hii migomo ya madaktari wako wanaonufaika kisiasa na wako wanaonufaika na matumbo yao. Huyu shetani Ulimboka Watz mkimfuatilia kwa undani kuna faida anazozipata kutokana na hii migomo,kama sio mfanyakazi wa serikali kwa nini ashupalie migomo ya madaktari wa serikali na si porivate hospital,kwani huko private hospital wanawalipa kiasi hicho wanachokitaka,huko wanaambiwa tunakupa kiasi hiki hutaki ondoka. sasa hawa huko serikalini ni wezi wa dawa,vifaa vya hospital kutumika kwa maslahi yao na mambo mengi tu.SHETANI ULIMBOKA MUNGU ATAKULAANI ZAIDI HAYO MAFIGO YAKO KILA MARA YAKULETEE MATATIZO,UPATE KISUKARI ,PRESSURE,KANSA NA MARADHI MENGI YANAYOWATESA WENGINE ILI UONE TABU WANAZOZIPATA HAO MNAOGOMA KUWAHUDUMIA KWA AJILI YA PESA ZA ANASA
ReplyDeleteKwa kweli! WATANZANIA WENGI TUMEJAZWA UNGA WA NDERE VICHWANI MWETU KIASI KUWA TUMESHINDWA KUKEMEA MAOVU NA HIVYO WATAWALA WANAFANYA TU KILE WANACHOKIPENDA! HIVI HAWA WATU WAMESHINDWA KUONA NYEUSI KAMA NYEUSI NA HIVYO KUFANYA MAOVU WANAVYOPENDA: WANAINGIA DILI NA MABEPARI KUTUFANYA TUWE MASKINI MILELE! MAFISADI WANAENDELEA KUSIFIWA BILA AIBU HUKU WAVUJA JASHO HATUTENDEWI HAKI NA HATUNA MTETEZI!SASA UTAWALA WETU UMEKUWA WA KIIMLA HATA WA YULE HITLA AFADHALI, WANYONGE TUNAULIWA KILA SIKU KAMA KUKU, TIZAMA CHENGE ALINYONGA WAWILI, AKALIPA VIJISENTI SABINI NA ANAPETA BILA AIBU NA WATAWALA HAWAONI SHIDA,BADO NI MJUMBE WA NEC NA MBUNGE!WAPO WALIOUWA KWA BAHATI MBAYA LAKINI WANASOTA RUMANDE HUU MWAKA WA KUMI HATA KESI HAIJASIKILIZWA KISA 'NO VIJISENTI',WATANZANIA HAWA WA AJABU HAWAYASEMEI WANASHABIKIA UNYAMA ALIOTENDEWA ULIMBOKA, JAMANI UBEPARI KWELI NI UNYAMA MWALIMU NYERERE ALITUFUNDISHA.BILA SHAKA HAWA NI VIJIBWA VYA WAKUBWA WANAOWABWEKEA MABWANA ZAO;HEBU FIKIRIENI ELIMU INAVYODORORA ,HALI YA HOSPITALI ZETU HOI,WANANCHI HAWALI CHAKULA CHA MAANA, FEDHA ZETU ZINAFUJWA KWA ANASA NA TULIOWAPA DHAMANA LAKINI HAWA WALIOLEWA MAKOMBO YA MABWANA ZAO HAWAONI WANAENDELEA KUWAPIGIA CHAPUO WEZI NA WADHULUMATI WAKUBWA. SUBIRINI KIKOMBE CHA MUNGU KIKIJAA MTAONA UTAMU WA UDHALIMU WENU NAKISHA SIJUI MTACHEKEA MENO GANI. HIMA WATANZANIA TUWAKATAE VIBARAKA HAWA WANAOKEJELI UMASKINI TUNAOLAZIMISHWA NAO,TUKATAE MFUMO USIOJALI WANYONGE NA KUKUMBATIA UDHALIIMU, UFISADI, UBADHIRIFU,MAUAJI YA KINYAMA, UDIKTETA NA UKANDAMIZAJI. MWISHO WAO SI MBALI MUNGU AMENENA:FEDHA ZAO ZITAWALA KAMA KUTU NA KASRI ZAO ZITAWAANGUKI NAKUWAZIKA NA MWISHO HUO MCHUNGU UTAJIA KAMA MWIZI.KEMEENI UOVU WA WANA WENU, MSIJE MKAANGAMIA!
ReplyDeleteNikweli Bwana hapo umenena! hawa ni vijibwa tu vya Mabepari na vibaraka wenye njaa kali wanaonawa damu za wenzao na kula nyama za wavuja jasho wanaouliwa kila siku ili wawanyamazishe watu wasitafute ukombozi.mnaoona kitendo alichotendewa ulimboka ni sahihi hakika ndio mliohusika.Kamwe mtu mwema hufikiria la mwenzake kama lake. Haiwezekani wengine wanalala hai na wengine hoi we uone ni sawa sawa kama hupewi makombo ya mabepari.Daima asifuye mvua imamnyea. Nasma hivyo kwa sababu, kabla madaktari hawajagoma walito malalamiko yao na kusubiri ; walipoona kimya wa litahadharisha ili serikali izinduke iwasikilize, lakini kama kawaida ya serikali yetu huwa wanasubiri ZIMAMOTO AU HADI JAMBO LITOKEE na kukurupuka na vituko kama hivyo walivyomfanyia daktari! SASA ANAYE ONA MADAKTARI WANAOKESHA kila siku kuokoa maisha yetu HAWASTAHILI KUFIKIRIWA au ndo yale ya PUNDA AFE MZIGO WA BWANA UFIKE ATAKUWA SAWA NA WATESI WA ULIMBOKA. NA NAFIKIRI WANYAMAZE AU WANYAMAZISHWE. Hawana hoja ya kutusaidia Walalahoi....
ReplyDeleteDR ULIMBOKA IS THE KING OF SALVATION, AND HERRO EVEN JESUS DIED ON THE CROSS BECAUSE OF OUR SIN, HE CAME TO SHOW US THE WAY ON HOW TO TREAT EACH EVEN MOHAMMED WAS STONED TO DEATH, KING DAVID HAD TO FIGHT BATTLES UNTIL HE WON AND BECAME KING, LET THOSE WHO HAVE EYES AND EARS NOT TO SEE AND LISTEN THE VOICE OF SALVATION SOME CRIED FOR THEIR BELOVED WHO LOST THEIR LIFE BUT THOSE WERE THE SACIRIFICATION OF BLOOD TO CLEANS OUT OUR SINS EVEN WHAT HAPPENED TO DR HIS BLOOD USED TO SACIRIFY FOR OUR SINS AND BRING SALVATION SEE WHATG HAPPENED TO JOUNALIST DAUDI HIS WAS HE AMONG THE STRIKERS? BUT WAS KILLED WITH BABYLON AND HIS BLOOD STILL IS THE SACIRIFICATION FOR OUR SINS, WE TANZANIAN WE HAVE SIN AGAINST OUR LORD KING OF KING, WE HAVE TO REPENT AND DWELL OUR MINDS INTO HIS SALVATION AND GLORY.HATRED, HUNGER POVERTY CORRUPTION, GREED ARE FROM EVIL WHO EVER FIGHT AGAINST THOSE IS THE HERRO. DR IS THE HERRO THE TRUTH WILL COME TO REVIEW SOON OR LATER.STOP BEING FOOL MANDELA WAS JAILED FOR 27 YEARS AND ONE AMONG THE RESPECTED HERROS IN THE WORLD AND DO YOU KNOW HOW MANY DIED TO BRING THE SALVATION IN SOUTH AFRICA? NYERERE FOUGHT IDI AMIN DOU YOU HOW MANY DIED IN THE THAT BATTLE? HAVE YOU HEVER BLAMED NYERERE BUT STILL IS THE HERRO STOP BEING A STUPID FOOOL SHORT SIGHTED CRY FOR YOUR BELOVED YOU HAVE TO START THINKING WHAT WILL YOU DO FOR YOUR MY NATION BUT NOT WHAT MY NATION WILL DO FOR YOU. STOP THINKING BACKWARDS.GREAT KING DR ULIMBOKA AND READ ZABURI 17 JAH BLESS YOU AND PROTECT YOU FOR YOU CHOSE TO STAND FOR TRUTH AND YOU CRUCIFIED AND LAID DOWN THE STONE BUT YOU WERE RAISED AGAIN TO VERIFY THE POWER OF TRINITY PEACE AND LOVE BE UPON YOU,WE WILL LEAVE TO OUR CREATOR WHO WILL STRIKE DOWN AND PERISH THE WICKED ONES FROM THEIR EVIL KINGDOM
ReplyDelete