17 August 2012
Tatizo la uchafu jijini ni aibu kwa wahusika
Na Neema Malley
CHANGAMOTO inayoikabili miji mikubwa nchini ni mrundikano wa takataka maeneo yasiyo rasmi na kuhatarisha kuhatarisha afya ya wakazi wake.
Majiji ya Dar es Salaam, Mbeya na Mwanza ni miongoni mwa miji mikubwa yenye wakazi wengi ambao huzalisha takataka kwa wingi.
Kutokana na idadi ya watu kuongezeka uzoaji taka huwa tatizo kwani watu hukosa maeneo ya kutupa taka na kuziweka sehemu zisizo rasmi.
Ukipita maeneo tofauti mitaani imekuwa ni kawaida kukutana na rundo la takataka na kutengeneza dampo katika makazi ya watu.
Ni wazi kuwa katika jiji hili kuna upungufu wa vifaa vya kuwekea taka hasa katika vituo vya mabasi, viwanja vya mpira na maeneo yenye shughuli za kibiashara ambazo huwa na mkusanyiko wa watu.
Tatizo hili limetokana na mpango mpya ulioanzishwa na halmashauri kumiliki jukumu la ukusanyaji wa takataka na kusimamisha utaratibu uliokuwa unatumika mwanzo ambapo kila mwananchi aliwajibika kutupa taka.
Mpango huu umekuwa ni chanzo cha uchafuzi wa mazingira kutokana na waendeshaji wa mradi huo kushindwa kuuendesha na kusababisha takataka kurundikwa na kukaa muda mrefu bila kutolewa.
Kwa upande mwingine naweza kusema kuwa mpango huu umeshindwa kufanya kazi na ni chanzo cha jiji kuonekana chafu kuliko uliokuwa unatumika awali kutokana na mpangilio wake kutoeleweka.
Baadhi ya watu wamekuwa wakipita mitaani wakitangaza kuwa watu wachukue takataka kupeleka katika gari watu wakifika wanakuta hakuna gari na kuamua kuziacha katika eneo hilo.
Wakati mwingine wanatangaza siku ya kumwaga takataka lakini inapofika hakuna kinachoendelea.
Kinachosikitisha gari la kusombea takataka halipiti siku hiyo linaweza kupita hata baada ya siku mbili au tatu mbele hivyo kuwasababishia kero wakazi wa eneo.
Utaratibu wa awali wa utupaji taki uliowahusisha wananchi walijipangia utaratibu mzuri ambapo ilikuwa ni vigumu kukuta takataka zikizagaa hovyo kwani walijiwekea mpango mzuri uliosaidia kufanya kazi hiyo kwa ufanisi mkubwa.
Kwa sasa licha ya wananchi kuingia gharama kubwa juu ya uendeshaji mzima wa huduma hii hali imekuwa mbaya na kuhatarisha afya za wananchi.
Pia wanapoweka uchafu kwenye kwenye mitaa yetu huweza kutuletea madhara kwa afya za watoto wetu kwani watoto hugeuza kuwa sehemu ya kuchezea.
Nionavyo, wahusika wa mpango huu watengeneze utaratibu mzuri ukiwepo wa kubeba takataka kwa wakati ambapo utaondoa kero ya madampo mitaani na kulifanya jiji kuwa katika hali ya usafi.
Aidha wanaweza kuteua sehemu moja ambayo ni mbali na makazi ya watu ambapo watu watatakiwa kupeleka takataka huko kabla ya gari halifika kuchukua uchafu huo kuliko kuzikusanya mitaani huku haijuliani na lini gari hilo litapita.
Pia waondoe utaratibu mzima wa kuchukua takatata kwa wiki mara moja ambayo ni ratiba ya maeneo mengi waongeze siku za kuchukua takataka kwa wiki angalau wabebe mara mbili kwani muda mwingine mtu anajaza takataka kabla hata cku ya kuchukua.
Ni aibu kwa jiji hili ambako viongozi wengi na ofisi nyingi za serikali zipo linalopaswa kuwa kioo cha taifa kwa usafi kuwa kitovu cha kipindupindu ugonjwa unaotokana na uchafu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment