16 August 2012

Sumsung kutoa mafunzo ya michezo




Na Mwandishi Wetu, Monduli

KAMPUNI ya Samsung Electronics imepanga kutoa msaada wa sh. milioni 144, ili ya kusaidia Shule ya Msingi Ilmorijo na Shule ya Michezo ya Sekondari ya Winning Spirit za Wilaya ya Monduli, Arusha.

Akizungumza mjini Mondoli jana Makamu wa Rais wa Sumsung Choi Woo-Soo, alisema shule ya kuendeleza vipaji vya michezo ya watoto ya Winning Spirit, itapata nafasi ya kutoa mwanafunzi mmoja ambaye atalipiwa gharama za masomo na kupewa mafunzo ya michezo hasa riadha.


Alisema mkakati huo utasaidia kuandaa watoto wenye vipaji, ambao watapata usaidizi wa Samsung na kuwa wanamichezo bora nchini na duniani kwa ujumla.

“Tumejidhatiti kuweka tofauti ya wazi kabisa katika maeneo ambayo wateja wetu wanaishi,” alisema Woo-Soo.

Alisema huo ni uthibitisho wa miradi waliyoianzisha katika maeneo mengi ya bara la Afrika katika sekta ya elimu, michezo na kuunganisha vijiji na mahitaji ya kimsingi ya jamii.

Makamu huyo alisema mradi wa programu hiyo pia umeanzishwa katika nchi za Afrika Kusini, Kenya na Nigeria kwa lengo la kutatua tatizo la upungufu wa wataalamu na mafundi katika Afrika kwa kutoa mafunzo ya ufundi na michezo kwa vitendo kwa wanafunzi wa shule za sekondari.

No comments:

Post a Comment