28 August 2012

SUMATRA kukusanya maoni ya wadau kuhusu kanuni za usafirishaji



Na Grace Ndossa

MAMLAKA ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA), leo itakutana na wadau wa sekta ya usafirishaji abiria kwa njia ya barabara, na wananchi ili kukusanya maoni yao kuhusu mapitio ya kanuni za ufundi, usalama na viwango vya ubora wa huduma kwa magari ya abiria.


Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari Dar es Salaam jana na Ofisa Mawasiliano wa SUMATRA, Bw. David Mziray, alisema wadau hao watapitia kanuni za leseni ya usafirishaji magari ya abiria ya mwaka 2007, kanuni za ufundi, usalama na ubora wa huduma za za mwaka 2008 ili kuangalia kama zinahitaji maboresho.

“Mkutano huu utasaidia kupata yao baada ya SUMATRA kufanya mapitio ya kanuni za leseni ya usafirishaji za mwaka 2007, na kubaini zinahitaji maboresho,” alisema.

Katika mkutano huo, mamlaka hiyo itawasilisha rasimu ya mapitio ambapo wadau watapata fursa ya kuchangia mapendekezo yao hivyo aliwaomba wadau na wananchi kujitokeza kwa wingi ili waweze kutoa maoni yao.

No comments:

Post a Comment