31 August 2012

Redds Miss Mwanza, Mashariki kivumbi


Na Mwandishi Wetu

SAFARI ya kuwania taji la Redd’s Miss Tanzania 2012 inaendelea kushika kasi, ambapo leo kutafanyika mashindano ya kumsaka Redd’s Miss Mwanza na kesho Redd’s Miss East Zone atapatikana Morogoro.


Michuano ya Redd’s Miss Mwanza 2012, yanatarajiwa kufanyika katika Ukumbi wa Yacht Club kuanzia saa 2 usiku ambapo warembo 16, watapanda jukwaani kuwania taji hilo ambalo linashikiliwa na Irene Karubaga.

Mashindano hayo yatasindikizwa na waimbaji nguli wa taarabu nchini Khadija Kopa, Mwanahawa Ally pamoja na wasanii wengine.

Akizungumizia mashindano hayo, Peter Omari ambaye ndiye anayeratibu alisema kiingilio kitakuwa sh. 50,000 kwa viti maalumu na sh. 20,000 kawaida.

Naye mratibu wa Redd’s Miss Kanda ya Mashariki, Alexander Nikitas alisema mchuano huo utakaoshirikisha warembo 12 utafanyika katika Ukumbi wa hoteli ya Nashera.

Warembo kutoka Mikoa ya Morogoro, Lindi, Mtwara na pwani ndiyo watakaowania taji hilo ambalo linashikiliwa na Loveness Flavia.

Alisema kiingilio katika mashindano hayo yanayodhaminiwa Redd's Premium Lager kitakuwa sh 20,000 kwa viti maalumu na sh 5,000, ambapo msanii Wanne Star na wengine watatoa burudani.


No comments:

Post a Comment