31 August 2012

Dstv waongeza chanel mpya



Na Victor Mkumbo

KAMPUNI ya Multichoice, imezindua baadhi ya Chanel mpya ambazo zitaanza kuonekana hivi karibuni.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Ofisa Habari wa Dstv Tanzania Barbara Kambogi, alisema wameamua kuzindua chanel mpya ambazo zitawafanya wateja wao kuangalia burudani mbalimbali.


Alisema chanel mpya, ambazo wameongeza zitakuwa zinaonesha vipindi vya burudani mbalimbali ikiwa ni pamoja na za watoto.

Barbara alisema vipindi hivyo vitakuwa vikionekana kupitia Dstv, ambapo vimegawanywa katika namba mbalimbali na vitakuwa vinapatikana kila siku.

Alisema chanel hizo zitaanza kuonekana kuanzia Oktoba mwaka huu na mteja atatafuta sehemu anayopa na kuweza kupata burudani zaidi.

Alisema baadhi ya chanel zitakuwa zinaonesha picha za matukio, vichekesho pamoja na ngoma.

“Tunatarajia baada ya uzinduzi huu wateja wetu watafurahia zaidi huduma ya Dstv, kutokana na ongezeko la chanel lenye vitu vingi tofauti na awali,” alisema.

No comments:

Post a Comment