31 August 2012
Mwanemti kutupa karata leo PARALIMPIKI
Na Amina Athumani
MWAKILISHI wa Tanzania katika michuano ya Walemavu ya Olimpiki (PARALIMPIKI) iliyoanza juzi jijini London, Uingereza Zaharani Mwanemti, leo anaanza kutupa karata yake ya kwanza.
Michezo hiyo ya walemavu huanza mara baada ya kumalizika kwa michezo ya Olimpiki, ambayo hufanyika kila baada ya miaka minne kama ilivyo.
Tanzania katika michezo hiyo ya inawakilishwa na Mwenemti, pekee ambapo atashiriki kategoria ya kurusha kisahani na tufe.
Michezo hiyo ambayo imeanza kuchezwa rasmi jana kwa michezo ya mpira wa kikapu, kulenga shabaha, kuogelea na baiskeli watu 80,000 walihudhuria katika sherehe za ufungunzi.
Kwa mujibu wa mtandao wa London Olimpiki wanamichezo 4,200 kutoka nchi 164 duniani, wanashiriki michezo hiyo ikiwemo Tanzania.
Michuano hiyo ya siku 11 imefunguliwa na Malkia wa Uingereza, Elizabeth ambapo mwanamichezo wa kwanza wa nchi hiyo aliyepata medali ya dhahabu Margaret Maughan, alipewa heshima ya kuwasha mwenge wa michezo hiyo kwa niaba ya wanamichezo wanaoshiriki michezo hiyo.
Katika michuano ya Olimpiki 2012 iliyomalizika Agosti 12 mwaka huu, Tanzania ambayo iliwakilishwa na wanamichezo sita ilirudi mikono mitupu.
wa upande wa Tanzania inashiriki michuano hiyo ikiwa na kumbukumbu nzuri ya siku chache zilizopita katika jiji hilo kufanya vibaya katika michezo ya Olimpiki iliyomalizika Agosti 12.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment