31 August 2012

Gadna G Habash sasa kurindima Times FM



Na Mwandishi Wetu

KITUO cha Redio Times FM, kinachokuja kwa kasi nchini jana kimemtangaza rasmi mtangazaji maarufu nchini, Gadna G. Habash kujiunga nao baada ya kukaa nje ya ulingo kwa muda mrefu.

Gadna kabla ya kujiunga na kituo hicho, miaka miwili iliyopita alikuwa mtangazaji mahiri katika kituo cha Clouds FM, ambako alipata maarufu kwenye kipindi cha Jahazi kinachorushwa kila siku jioni.

Akizungumza Dar es Salaam jana katika hafla ya kumtambulisha mtangazaji huyo Mhariri Mkuu wa Redio Times, Scolla Mazula, alisema Habash katika kituo hicho atatangaza kipindi maalumu cha Maskani kitakachokuwa kikirushwa kila siku saa 10 jioni hadi saa 1 usiku.

Habash ametambulishwa rasmi kuhamia Radio Times FM, baada ya kuwa nje ya kazi kwa takriban miaka miwili, tangu alipoondoka Clouds FM.

Naye Habash ambaye ni mume wake msanii mahiri nchini Judith Wambura Jay Dee, alisema kipindi chake kitazungumzia mambo mbalimbali ya jamii pamoja na burudani na michezo kila siku.

No comments:

Post a Comment