21 August 2012
Maofisa afya wadaiwa kupokea rushwa
Na Patrick Mabula, Kahama
BAADHI ya Maofisa Afya wa Halmashauri ya Mji wa Kahama, mkoani Shinyanga, wanadaiwa kujenga utamaduni wa kuomba na kupokea rushwa wanapotekeleza wajibu wao katika operesheni za usafi wa mazingira katika mitaa mbalimbali.
Madiwani wa mji huo, waliyasema hayo mwishoni mwa wiki katika kikao chao na kudai kuwa, tabia hiyo inafanywa na maofisa hao wakishirikiana na askari mgambo.
"Hawa maofisa pamoja na askari mgambo wanawaomba rushwa wafanyabiashara na mama lishe wanapokuwa katika operesheni ya kusimamia suala zima la usafi wa mazingira," alisema.
Diwani wa Viti Maalumu, Bi.Aoko Nyangusu, alisema maofisa hao wamekuwa kero kwa wananchi kutokana na vitendo vya kuomba rushwa wanapokuwa katika operesheni zao.
Bw.Abas Omari ambaye ni Diwani wa Kahama Mjini, alisema kitendo kinachofanywa na maofisa hao kinawafanya wananchi waichukie Serikali yao.
"Suala la usafi wa mazingira ni muhimu pamoja na hili la kuwaondoa wafanyabiashara katika maeneo ambayo hayaruhusiwi kisheria lakini lisiwe mradi wao wa kula rushwa," alisema Bw.Omari.
Kwa upande wake, Katibu Tawala wilayani hapa, Bw.Ernest Masanja, ametoa onyo kwa maofisa hao pamoja na askari mgambo wenye tabia hiyo na kuwataka waache mara moja.
"Jambo la msingi kila mmoja atekeleze wajibu wake bila kutumia lugha za matusi au kuomba rushwa kwa wananchi, lengo ni kuhakikisha mji wetu unakuwa safi muda wote," alisema.
Aliwaagiza askari mgambo kuwaondoa wafanyabiashara waliopo katika maeneo yasiyoruhusiwa bila kutumia nguvu kubwa, kuchukua bidhaa zao na kuwaomba rushwa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment