24 August 2012
Majenerali watatu JWTZ kuagwa leo
Na Mwandishi Wetu
JESHI la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), leo litawaaga Majenerali wake ambao wamestafu jeshi kwa mujibu wa sheria.
Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari Dar es Salaam jana na
Kurugenzi ya Habari na Uhusiano, Makao Makuu ya jeshi hilo Upanga, imesema sherehe ya kuwaaga Majenerali hao itafanyika katika Kambi ya Twalipo, kuanzia saa mbili asubuhi.
“Majenerali ambao wataagwa ni Maj Jenerali Miti, Maj Jenerali Ulomi, Maj Jenerali Kitundu na Maj Jenerali Kalembo,” ilisema taarifa hiyo na kuongeza kuwa, mgeni rasmi atakuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Davis Mwamunyange.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment