02 August 2012
Madai ya Walimu haya wezekekani-JK Adai haiwezekani walipwe fedha zote za watanzania *Asema serikali haijawapuuza bali kipato ndio tatizo
Na Imma Mbuguni
RAIS Jakaya Kikwete amesema, Serikali inawajali walimu wote pamoja na kutambua mchango wao kwa maendeleo ya Taifa lakini madai yao ni vigumu kuyatekeleza kama wanavyotaka.
Alisema yeye mwenyewe amekuwa mstari wa mbili kutetea haki na masilahi ya walimu lakini madai yao kwa sasa ambayo ndio chanzo cha mgomo unaoendelea katika mikoa mbalimbali nchini ni makubwa kupita uwezo wa Serikali.
Rais Kikwete aliyasema hayo Ikulu, Dar es Salaam jana wakati akizungumza na Wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari.
Alisema kama walimu wataongezewa mishahara kwa asilimia 100 kama wanavyotaka, pamoja na madai mengine Serikali italazimika kutumia zaidi ya sh. trilioni 6.5 kwa kuwalipa mishahara wakati pato zima la Taifa sh. trilioni nane.
Alisema Serikali haikupuuza madai yao bali imeyachukulia kwa uzito wake na kwamba suala hilo kwa sasa lipo mahakamani baada ya mazungumzo ya Serikali na viongozi wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), kushindikana katika hatua za awali.
“Wenzetu tuliwaeleza uwezo tulionao lakini hawakukubali, wakaenda Baraza la Usuluhishi na sisi tukaenda na kuwaambia tuendelee na mazungumzo kama tulivyoanza awali ili kufikia muafaka lakini walikataa,” alisema Rais Kikwete.
Alisema CWT waliendelea na dhamira yao ya kutaka kugoma ambapo Julai 27 mwaka huu, walitoa notisi ya saa 48 kwa Katibu Mkuu Kiongozi juu ya kusudio la kugoma kuanzia asubuhi ya Julai 30 mwaka huu.
Hata hivyo, Rais Kikwete alisema Serikali ilipigwa chenga ya mwili baada ya CWT kutoa taarifa ya mgomo siku za mapumziko.
“Hii ni sawa na mtu kukupeleka polisi siku ya Ijumaa, anataka ulale Jumamosi na Jumapili ili kama ni dhamana upewe Jumatatu,” ndivyo walivyofanya walimu ili kutimiza dhamira yao.
“Serikali bado ina nia nzuri na haijayapuuza madai yao kama wanavyoamini, walimu ambao wanaendelea na kazi wasisumbuliwe na wale waliogoma, Serikali ipo makini kuhakikisha usalama wa walimu ambao hawajagoma,” alisema Rais Kikwete.
Alisema haiwezekani walimu walipwe fedha zote za Watanzania na kubaki sh. trilioni mbili ambazo hazitoshi kuhudumia sekta nyingine za maendeleo kama barabara, afya na vitabu hivyo kuna umuhimu wa kuzigawa pesa hizo ili kuhakikisha kila sekta inapata mgawo kutokana na hali ilivyo.
Hadi jana, mgomo wa walimu uliingia siku ya tatu ambapo Mahakama Kuu, Divisheni ya Kazi, inatarajia kutoa uamuzi wake leo kuhusu hatima ya mgomo huo.
Wanafunzi wa shule mbalimbali nchini, wameonekana mitaani wakizurura kutokana na mgomo unaoendelea pamoja na kuwepo madai kuwa, walimu waliogoma wanashinikiza wanafunzi kulala barabarani na wengine kuandamana wakidai haki ya kupewa elimu.
Mwisho.
Alisema walimu walioamua kufundisha wasibughudhiwe na waliogoma wanaojisikia kugoma wasiwasumbue wasiotaka kugoma.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Hii migomo ya mara kwa mara itatufikisha wapi?. Mara madaktari mara walimu na mwisho itafikia sekta nyingine kama za majeshi yote, Sekta za uchumi, mawasiliano, miundo mbinu na nyiginezo kwa ujumla.Serika litafakarini hili tusije tukawa Somalia ya pili
ReplyDeleteNa sisi wa sekta nyingine kama majeshi n.k. tugome ?
ReplyDeletewanajeshi watagoma kwa nini wakati ..mshahara na marupurupi ni mazuri
Deletenashangaa serikali kulalamika kuwa ilipigwa chenga ya mwili, hawakumbuki kuna mwaka serikali walienda mahakamai kuzuia mgomo siku ya weekend na mahakama ikazuia mgomo huo wa walimu siku ya jumapili usiku!!???
ReplyDeleteWAALIMU MULIKWISHA ANZA MGOMO ZAMANI MBONA WANAFUNZI WENGI HAWAJUI KUSOMA NA KUANDIKA NI HAO WACHACHE 6000 WALIOBANIKA BAADA YA KULAZIMISHA KUINGGIA SEKONDARI KAMA VALUE FOR MONEY ITAZINGATIWA WAALIMU WATATAKIWA KUTOA HESABU
ReplyDeleteNi kweli madai ya walimu ni ya msingi lakina je? huu umeanza leo jana ama juuzi? Kiwango cha elimu kimeshuka kiasi cha kutisha hadi wanafunzi wanakwenda sekondari wakiwa hawajui kusoma na kuandika?
ReplyDeleteHIVI WATAALAMU WA UCHUMI TANZANIA WAKO WAPI HII NI AWAMU YA PILI YA RAIS KIKWETE KWELI KUNA HAJA YA KUJIPENDEKEZA KWA WAPIGA KURA KWANI ATAGOMBEA TENA?? WATANZANIA WENGI WANAZURURA HAKUNA UZALISHAJI WA AINA YOYOTE SI VIWANDANI SI MASHAMBANI KAZI ILIYOKO NI KUCHUUZA BIDHAA ZA ULAYA NA ASIA AIBU KUBWA JE ULAYA NA ASIA WANACHUUZA BIDHAA ZA TANZANIA??NI LINI TUTAKOMA KUWA SHAMBA LA MALIGHAFI YA VIWANDA VYA ULAYA NA ASIA NI LINI TUTAACHA KUWA SOKO LA BIDHAA ZA ULAYA NA ASIA NI KWELI RASILIMALIWATU NI SIFURI HIVI BUNGENI WANAJADILI NINI MBONA SIWAELEWI WANACHOSHAURI SERIKALI NI KUPRINT HELA KILA WIZARA IPEWE NYINGI IWEZE KULIPA MISHAHARA MIKUBWA NA KUTEKELEZA MIRADI MBALIMBALI USHAURI HUU HAUNA TOFAUFI NA ULE WA IDDI AMIN WA UGANDA NA MUGABE WA ZIMBABWE WALIOPRINT NOTI NA KUSABABISHA MFUMUKO WA BEI NA KUSHUKA KWA SARAFU TUWAELEZE WATANZANIA WAKULIMA NA WAFANYAKAZI KUWA KILA MMOJA AJILIMIE CHAKULA CHAKE CHA KUMTOSHA MWAKA MZIMA KUPIGA DEBE SI KAZI HALALI WAPIGA DEBE WAONDOLEWE KWA NGUVU ZOTE WANA SIASA ACHENI KUDANGANYA WATANZANIA UKIPRINT FEDHA NYIGI NA CHAKULA NA BIDHAA HAKUNA WEHU KAMA SI UKICHAA
ReplyDeleteIKIWA RAIS WETU ANASEMA KUWA MADAI YA WAALIMU HAYAWEZEKANI NA KIPATO CHA SERIKALI NI KIDOGO, BASI WAALIMU TUMIENI SILAHA YENU KUBWA YA KURA ZENU 2015 MUWAPIGIE KURA RAIS NA WABUNGE AMBAO WANA UWEZO WA KUTUMIA VIZURI RASLIMALI ZA NCHI ILI WAWALIPE MADAI YENU.WAWE WA KUTOKA CCM AU VYAMA VYA UPINZANI.
ReplyDeleteNINAWAPONGEZA KWA KUTAMKA KUWA MTATUMIA KURA ZENU NA ZA WASHABIKI WENU ILI KUWAPATA VIONGOZI WENYE KUJALI SHIDA ZA WAALIMU NA WANANCHI KWA UJUMLA
WALIMU WAANZE KWA VITENDO MAPEMA KWA KUWAHAMASISHA WANAOWAJALI. WAALIMU WAKO VIJIJINI NA MIJINI . MNA WAFUASI WENGI WAKIWAKO WANAFUNZI WAZAZI, WABUNGE, WANA TUCTA, WANACHAMA WA HIFADHI YA MIFUKO, MADAKTARI, MAPROFESA N.K.
IKIWA SERIKALI ITAKUWA INATUMIA MAHAKAMA AU VITISHO KUWAKANDAMIZA NA KUWANYANYASA, BASI, TUMIENI SILAHA HII YA KURA AMBAYO NI KALI KULIKO MIGOMO, MAANDAMANO, GESI YA KUTOA MACHOZI, VIRUGU N.K.
MIGOMO SIO MIZURI KWA KUWA INAWAUMIZA WANANCHI NA WAALIMU WENYEWE KULIKO VIONGOZI WANAOTUONGOZA AMBAO WANABAKI WAKIWASANIFU. MKIWATOA MADARAKANI KWA KURA ZENU, KAMWE HAWAWEZI KUWACHEZEA WANAVYOWAFANYA.
MLIVYOWATISHIA KWA SILAHA YA KURA SI AJABU SERIKALI IKAWAFIKIRIA. TISHIO LA SILAHA YA KURA NDILO LILILORUDISHIA WANANCHI WA ARUMERU MASHARIKI MASHAMBA YAO YALIYOKWISHA KUPORWA NA SERIKALI.
SILAHA YA KURA INAWATISHA HATA KINA OBAMA.
Waalimu wote mliocompetent acheni kazi hiyo mtakufa maskini. wenzenu tilikimbia, shauri yenu na uzalendo wenu
ReplyDelete