30 August 2012
Kutambulisha mwanamuziki mpya kesho
Na Mwandishi Wetu
BENDI ya muziki wa dansi Mashujaa "Wana Kibega', kesho wanatarajia kufanya onesho maalumu kwa ajili ya kumtambulisha mwanamuziki mpya ambaye hata hivyo uongozi wa bendi hiyo haujaweka wazi bedndi atakayotokea.
Akizungumza Dar es Salaam juzi Meneja wa Mashujaa, Martin Sospeter alisema utambulisho huo utakuwa wa aina yake kutokana na kwamba wataangusha shoo ya nguvu.
Sospeter alisema kila kitu kimekamilika ila kinachosubiriwa ni muda ufike ili waweze kuwajibika katika kutoa burudani.
"Tumeamua kufanya Suprise kwa wapenzi wetu watakaokuja kuona onesho letu ambalo ndiyo tutamtangaza mwanamuziki wetu mpya ambaye ataanza rasmi kazi usiku huo katika Ukumbi wa Business," alisema Sospeter.
Wanamuziki wengine waliojiunga ndani ya mwaka huu ni Charles Gabriel 'Chaz Baba', Lilian Tungaraza 'Lilian Internet', Soud Mohamed 'MCD' na Ali Akida ambao wote wametoka The African Stars 'Twanga Pepeta' na mwingine John Saulo 'Sauko Fagason' aliyekuwa Extra Bongo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment