30 August 2012
Wawili 'wavuta mkwanja' Mwanza
Na Mwandishi Wetu, Mwanza
KAMPUNI ya vinywaji baridi ya Coca-Cola ya Nyanza Bottlers, imewazawadia washindi wa promosheni ya 'Vuta Mkwanja' zawadi ya fedha taslimu.
Washindi hao ni Peter Cosmas, mkazi wa Wilaya ya Chato, Kagera aliyeshinda sh. milioni moja na Ndelekwa Paranjo kutoka Nyakato, Mwanza aliyeshinda sh. 100,000.
Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa zawadi, Cosmas ambaye ni mfanyibiashara alisema amejisikia furaha kuwa mmoja ya washindi wa Vuta Mkwanja.
“Nilikuwa nasikia watu wanajishindia zawadi mbalimbali kwa kunywa soda jamii ya Coca-Cola. Na mimi nikiwa ni mtumiaji mzuri wa kinywaji hicho, nilikuwa natamani kuwa mshindi," alisema.
Naye Meneja Masoko wa Nyanza Bottlers, Alfred Malandu alitoa wito kwa wateja wa Coca-Cola kuendelea kunywa soda za Coca-Cola, kwa kuwa bado zawadi zipo nyingi.
Promosheni ya Vuta Mkwanja na Coca-Cola, ilizinduliwa Julai mwaka huu na inatarajiwa kuendelea hadi Septemba mwaka huu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment