21 August 2012

Kavumbagu, Bahanuzi kazi moja kwa Lyon leo *Tegete 'amulikwa tochi'


Zahoro Mlanzi

MABINGWA wa Kombe la Kagame, timu ya Yanga leo inashuka uwanjani kuumana na African Lyon katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa ukaopigwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10 jioni.

Viingilia katika mechi hiyo ni Viti Maalum A (VIP A) ni sh. 15,000, VIP B ni sh. 10,000, VIP C ni sh. 7,000, viti vya machungwa ni sh. 5,000 na mzunguko ni sh. 3,000.


Akizungumzia mchezo huo, Kocha Mkuu wa Yanga, Tom Saintfeit alisema atachezesha kikosi chake chote ili kutoa nafasi kwa wachezaji wapya waoneshe viwango vyao.

"Tuna wachezaji wapya kama Didier Kavumbagu ambaye nilimuona katika michuano ya Kagame lakini sasa tunaye hapa klabuni, hivyo ni nafasi nzuri kwake kudhihirisha kiwango chake," alisema Saintfeit.

Akizungumzia kuhusu mshambuliaji, Jeryson Tegete alisema ni mchezaji mzuri kwa jinsi anavyomuana mazoezini, hivyo pia katika mechi hiyo atampa nafasi azidi kumuona.
Aliongeza kwamba baada ya mchezo huo, kikosi chake kitaondoka nchini kesho au keshokutwa kwenda Rwanda ambapo watacheza michezo kirafiki kabla ya kurejea nchini kwa ajili ya kuanza ligi kuu msimu ujao.

Mechi hiyo imeandaliwa na Chama Cha Mpira wa Miguu Mkoa wa dar es Salaam (DRFA) kwa kushirikiana na Kampuni ya Vannedrick katika mipango yake ya kuziweka sawa timu za mkoa huo ambazo zinashiriki Ligi Kuu Bara. Soka Mkoa wa Dar es

Awali Yanga ilikuwa icheze na timu ya Coastal Union lakini mchezo huo ulifutwa kutokana na kuwepo tatizo la uwanja ambapo Serikali imeruhusu uwanja huo utumike leo kwa ajili ya mchezo huo.

No comments:

Post a Comment