21 August 2012

Fennela aitaka Simba B kuepuka mihadarati



Na Zahoro Mlanzi

WAZIRI wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Fenella Mukangara amewataka wachezaji wa Simba B kutojihusisha na masuala ya uvutaji wa bangi ambao unaweza kusababisha kiwango chao kushuka.

Kauli hiyo aliitoa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam baada ya mechi ya fainali ya Sup8r kati ya Simba B na Mtibwa Sugar iliyomalizika kwa Simba kuibuka na ushindi wa mabao 4-3.


Alisema Simba imeonesha kiwango kizuri na ndio maana wametwaa ubingwa, hivyo ni vizuri wakaendelea na kiwango hicho hicho na kuepuka kujihusisha na dawa za kulevya.

“Naelewa wapo ambao hutumia dawa hizo, mimi ninawaomba waziache kwani sio nzuri kwao, wakiendelea kujitunza bila kujihusisha na vitendo vingine viovu tutakuwa na waxchezaji wazuri hapo baadaye," alisema Fenella.

Mbali na hilo, pia aliwapongeza waandaaji wa mashindano hayo benki ya BancABC kwa kusema ni mwanzo nzuri na kuziomba taasisi, mashirika na kampuni zingine zijitose katika mashindano mbalimbali.

Katika hatua nyingine, Makamu Mwenyekiti wa Simba, Geofrey Nyange 'Kaburu', aliwapongeza vijana hao kwa kazi nzuri waliyoifanya kwa kutwaa kombe na kutamba kwamba ni dhahiri sasa hawana shida ya kusajili nje.

No comments:

Post a Comment