17 August 2012

Madai ya Zitto, Ndugai alipuka *Asema anautumia vibaya ukumbi wa Bunge *Adai analifanya Taifa liamini uongo wake


Na Benedict Kaguo, Dodoma

NAIBU Spika wa Bunge, Bw. Job Ndugai, amemshukia Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Bw. Zitto Kabwe (CHADEMA), baada ya kushindwa kuwataja kwa majina viongozi wa Serikali aliodai wanahusika kuficha mabilioni ya fedha katika Benki za Uswisi.


Akizungumza na Majira nje ya ukumbi wa Bunge, mjini Dodoma jana, Bw. Ndugai alisema baadhi ya wabunge wanautumia vibaya ukumbi wa Bunge kwa kutoa tuhuma nzito bila kuzifanyia utafiti.

Alisema hali hiyo inalifanya Taifa liamini uongo huo ambapo hivi sasa Bunge linaangalia uwezekano wa kuzifanyia marekebisho kanuni zake ili kuwabana wabunge wenye tabia ya kuzungumza uongo na kupakazia wengine bila kuwa na ushahidi.

Aliongeza kuwa, Bw. Kabwe katika katika hotuba yake kama Msemaji wa Kambi ya Upinzani kupitia Wizara ya Fedha, alisema viongozi wa Serikali wamechota mabilioni ya fedha na kuyaficha katika Benki ya Uswisi huku akisita kuwataja kwa majina hivyo kusababisha Taifa kubaki njia panda.

“Kumezuka tabia ya baadhi ya wabunge kutumia vibaya ukumbi wa bunge na kutoa taarifa ambazo hawakuzifanyia utafiti wa kutosha hivyo kusababisha maswali mengi kwa wananchi.

“Mbunge anasimama na kusema kuna mabilioni ambayo yamechotwa na kufichwa katika Benki za Uswisi na viongozi wa Serikali lakini hawataji kwa majina au kiasi halisi cha fedha hizo...amezichota wapi, huku ni kujenga utamaduni wa kutuhumu, tabia hii imeanza kujengeka hapa nchini jambo ambalo zi zuri hata kidogo,” alisema Bw. Ndugai.

Hata hivyo, wakati Bw. Kabwe akiwasilisha hotuba yake bungeni, alisema kama kama Serikali itashindwa kuwataja kwa majina viongozi hao pamoja na wafanyabiashara wakubwa ambao wameficha fedha hizo, kambi hiyo itawataja.

Bw. Ndugai alidai kushangazwa na msimamo wa Bw. Kabwe na kusisitiza kuwa, kwanini asiwataje kwa majina pale pale kama si kutumia vibaya ukumbi wa Bunge kulingana na kinga zilizopo.

“Kama kweli Bw. Kabwe alikuwa na nia njema ya kile alichokisema kwanini hakuwataja moja kwa moja, mbele ya safari kuna umuhimu wa kupitia upya kanuni.

“Kitendo cha baadhi ya wabunge kuleta taarifa za uongo ambazo utafiti wake si mzuri, kinavunja heshima ya Bunge kwa kupakazia watu ili kuchafua upande mwingine uwe chama tawala au upinzani waonekane tofauti kwenye jamii,” alisema Bw. Ndugai.

Aliongeza kuwa ni vyema wabunge kama kuna jambo ambalo halijafanyiwa uchunguzi wa kina likaachwa badala ya kulizungumzia ndani ya Bunge.

“Huwezi kuitaka Serikali ijishughulishe na mambo ambayo haiyajui, yeye ndiye ameyaleta sasa kwanini asiyaseme badala ya kutaka maelezo,” alisema Bw. Ndugai.

15 comments:

  1. we pimbi kwelikweli...wewe kama mwenyekiti kwa nini usingestopisha hotuba yake then ukamwambia ataje hayo majina kama unalijua hilo?..By the way Zitto siyo mwanzilishi, ilaumu serikali ya urusi kwani wao ndyo waliofichua siri hiyo, je na wewe unaamini kuwa hyo issue ni uzushi? na kama Unaamini hivyo unafikiri hizo fedha zimefikaje kule wakati huku mnasema serikali haina fedha ya kuwalipa madaktari na walimu madai yao?

    ReplyDelete
  2. Hah hah haaaa! Lile gazeti lililotoa ushahidi kwa kuweka wazi mlolongo wote wa ushahidi wa mawasiliano ya simu kabla, wakati wa, na baada ya kumkamata na kumtesa ULIMBOKA si mlilifungia? Mlitaka atoe ushahidi ili mkamkate kucha zake kule kwenye msitu wa Mabwe Pande?

    Lazima mtakuwa hamfikirii ninyi. Nanyi mtakatwa kucha na kuminywa sehem seheeem siku ikifika.

    Jiniaaaaaz! Popkorn

    ReplyDelete
  3. TUACHE UJINGA WABUNGE WENGI NI MBUMBUMBU WA KUTAFUTA TAARIFA KWENYE MTANDAO TUACHE KUPOTOSHA WATANZANIA NIMESHANGAA KUONA MATAIFA KUMI YENYE WIZI WA KUTISHA NI YALE YENYE UCHUMI IMARA: CHINA $2.18 TRILION, RUSSIA $427 BILLION, MEXICO $ 416 BILLION, SAUDI ARABIA $ 302 BILLION, MALAYSIA $ 291 BILLION,UNITED ARAB EMIRATES $ 276 BILLION, KUWAIT $ 242 BILLION, VENEZUELA $ 157 BILLION ,QATAR $ 138 BILLION NA TAIFA LA KUMI NI NIGERIA $ 130 BLLION IWAPO HIZI NI CHANGAMOTO ZA UTANDAWAZI UNAOATHIRI HATA MATAIFA MAKUBWA SEMBUSE MBUMBUMBU WA TANZANIA LAUMUNI UTANDAWAZI IKIMBUKWE KINACHOWAANGAMIZA WATANZANIA NI UTANDAZUZU NA UTANDAWIZI

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mimi mara nyingi nimesema sitajihushisha na siasa kwa sababu siasa ni sehemu ya uongo .

      Nasema hivyo kwa sababu mbunge kabla hajachaguliwa kitu cha kwanza ni kutunga ni jinsi gani atakavyowadanganya wananchi kama siyo sahihi kutumia neno hilo basi nitumie kuwashawishi ili wakubaliane na hoja zake

      Lakini baada ya kuingia bungeni kama mbunge huyo ni smart akaweza kuwashawishi wafadhili au serikali basi atakuwa ameshinda na azma yake anaweza kuitekeleza pale atakapotekeleza mradi alioahidi/ushawishi

      Aidha tumeona wabunge wengi wakishirikiana na mawaziri kwa ajili ya kufanya miradi kadhaa au kuishauri serikali kufanya miradi kadhaa.

      Mingine ina manufaa kwa Taifa lakini mingine ni ya uhujumu uchumi tuangalie Tanesco ni wabunge wangapi na mawaziri wangapi wanaohusika na sakata la uhujumu uchumi kupitia Tannesco ni wengi sana wengine hata hawatajwi wala hawatakiwi kutajwa kwani ni aibu

      Lakini ni nini kinachowaumbua ni mabadiliko alipokuwa kabla wananchi hawajamchagua walikuwa wanamjua anavyokula anavolala, lakini ghafla bin vuu umepata ubunge amepata uwaziri mabo yanabadilika sio yeye tena , akiulizwa mbona akauti yako huko uswis ina mabilion anasema mbona ni vijisenti tu

      Nini maana yake amefikia pakubwa kama takwimu za hapo juu zinavyoonyesha. Kama alivyosema mtoa hoja hapo juu utandawazi ndio unaoangusha. Kila kitu kipo hadharani wenzetu hawafichi wale.

      Ona kwa mfano swala la rada waliona wanaumbuka hao wakubwa huko ughaibuni wakaona ni vyema wazirudishe hizo bilion 73 lakini wakaweka sharti kwamba mkanunue vitabu kwao , jee inaingia akilini hiyo au ni njia nyingine ya kuzichukua

      Unapoomba ubunge unatakiwa uwe kama Mchungaji anayechunga kondoo ,kondoo wako wakishiba ndiyo furaha yako kesho utauza manyoa ya kondoo / utapata sufi nzuri lakini ukitaka kula hata huo mradi wa kondoo hata hao waumini hutawaona tena kanisani watakimbia

      Wabunge tujifunze kusema na kusimamaia ukweli kama enzi za mwalimu Juius Kambarage Nyerere
      Mungu ibariki Tanzania na bunge letu

      Delete
    2. MHARIRI ACHA UANAHARAKATI/UBABE

      Delete
  4. ZIKO TAARIFA PIA KWA KIPINDI CHA MIAKA 2000- 2009 NCHI ZILZOONGOZA KWA KUTOSHWA FEDHA NI KAMA IFUATAVYO:1.CHINA $2.74 TRILION , 2. MEXO $540 BILLION, 3. RUSSIA $ 501 BILLION, 4.SAUDI ARABIA $ 380 BILLION,5. MALYSIA $ 350 BILLION, 6.UNITED ARAB EMIRATES $ 296 BILLION, 7.KUWAIT $ 271BILLION, 8.NIGERIA $ 182 BILLION,9. VENEZUELA $179 BILLION 10.QATAR $ 175 BILLION 11.POLAND $162 BILLION,12..INDONESIA $ 145 BILLION ,13. PHILIPINES $ 142 BILLION 15.KAZAKHASTAN $ 131 BILLION ,16.INDIA $ 128 BILLION ,17. CHILE $97.5 BILLION 18.ARGENTINA $ 95.8 BILLION 19.SOUTH AFRICA $ 85.5 BILLION ,20. TURKEY 79.1 BILLION HAYA NI MATAIFA YENYE AKILI DUNIANI BADO UTANDAWAZI UNAWAIBIA TENA MIAKA MINGI ILIYOPITA NASHANGAA KIPOFU KAONA MWEZI ANADANGANYA MBUMBUMBU WENZAKE BUNGE LA TANZANIA KAMA BUNGE LETU KUNA RASILIMALIWATU WAPAMBANE NA SERA CHAFU ZISIZO NA UTU ZA IMF NA WB ZINAZOIMARISHA UTANDAZUZU NA UTANDAWIZI HATUNA WABUNGE BALI MAZUZU .

    ReplyDelete
  5. Na We Ndungai Vipi. Badala ya kuchukulia uzito wamwambia atoe Majina. Vipi wewe. Umo ndani au wazidi kufunga Njia. Kwa sasa mtashindwa tu. Kama mnataka kumchafua Zito tena, hamwezi. Mageziti ya nje yaliyotoa Habari mbona hukanusha. Mali za Iran je.
    Wezi wakubwa serikali ya Tanzania.

    ReplyDelete
  6. SERIKALI ISIJE KWA VITISHO. TENDA KAZI SAFI UTAHESHIMIKA.POROJO WEKA MBALI. KAMA UNAELIMU BORA, SIKILIZA, TAFAKARI, NA UJUE WEWE NI MTUNISHI WA WATU.WAMTISHA KIONGOZI MWENZAKO KAMA MTOTO. TUNAOMBA SERIKALI ISIWAPOTOSHE WATANZANIA NA CHUKULIENI KAZI ZENU KWA MAKINI.MNALIPWA NA WATU KWA MANUFAA YA UMA, SI KUZURUMU, SI KUTISHA, BALI RUDISHENI HADHI YA NCI HII.MSIWEKE VIKWAZO. WAACHIENI WENYE ELIMU< NA EWEZO WA KUENDELEZA NCHI.
    BADO MNA YA KIZAMATI., HAKUNA UBWANA WALA UTWANA.
    JE UNAJUA HIYO?

    ReplyDelete
  7. Ndugai mkakati wako wa kutaka Uspika 2015 unakugeuza kituko, utadhani hujaenda shule. Bahati yako mbaya bunge la 2015 halitakua la CCM hata ukifanyia upinzani vitimbwi kiasi gani. Kwanza hata huo ubunge kwa mtindo huu unaweza usipate. Speaker anatakiwa kuwa impartial. Sasa unataka kurekebisha kanunu zinazoheshimika na mabunge yote ya kidemokrasia kwa sanabu ya kumthibiti mtu mmoja. Wewe pimbi kweli.

    ReplyDelete
  8. IWAPO CHINA WANATUMIA HUKUMU YA KIFO KWA MAFISADI INAKUWAJE NAO WAIBIWE?? HAINGII AKILINI KUWA NI RAHISI KUWATAJA TU WATU BILA USHAHIDI KWA KUWA SIASA NI MCHEZO MCHAFU ASIYE NA USHAHIDI AFIKISHWE MAHAKAMANI ILI KUJENGA SIASA SAFI "NITASEMA KWELI DAIMA FITINA KWANGU MWIKO"

    ReplyDelete
  9. Serikali ilisema kuwa inachunguza kuhusu fedha zilizofichwa Uswisi. Sasa kama serikali itatoa taarifa kuwa hakuna fehda zilizofichwa, ndipo Zitto na kambi ya upinzani wameahidi kuwataja walioficha fedha hizo. Sasa huyu Ndugai, hata kama mchuzi wa bendera ya ccm aliokunywa umemkolea kiasi gani; anawezaje kuhusisha msimamo huu wa kambi ya upinzani na Uwongo?. Ni uwongo upi huo? matusi dhihaka kejeli na uvivu wa kufikiri na upofu, alivyonavyo, ataendelea kuvitumia mpaka lini?

    ReplyDelete
  10. MAKINDA ACHA UDAKU
    KWELI MWANASHERIA MKUU ALISEMA KICHWA HAKIFUGI MYWELE TOA HILO WIGI LAKO TATUJUA AKILI ZAKO.
    ULIWAHI KUWAASA WABUNGE WAVUMULIVU KAMA ULIVYOKUWA WEWE KWANI HATUJUI SIRI ZAKO?
    NANI ALIKUWA ANAKUBEBA WEWE ULIKUWA MBUNGE NDIYO IMEPITA HATA USPIKA MAFISIDI WALIKUFUATA; CHAGUO LETU LILIKUWA MZEE SITTA NA WEWE ANGALIA UNAVYO VURUNDA BUNGENI WEWE NA NAIBU WAKO . ALIWAHI KUSEMA WATU WA KAWE ANGALIIENI MLICHOGAGUA, HEHEHEHE WATANZANIA KATIKA MAJIMBO YENYE WATU WENYE UPEO NA ELIMU NI KAWE NA UBUNGO SASA NYINYI UNAOIBA KURA KWA KANGA NA KOFIA MTAGILINGALISHA MNAFIKIRIKI KABLA YA KUBWATUKA

    ReplyDelete
  11. INASIKITISHA WAAFRIKA WALIVYOMBUMBU KUTUMIA RESEARCH KUTOKA WASHINGTON DC NA KUZIONA ZINA MASHIKO KWA NCHI ZA ULIMWENGU WA TATU IKIMBUKWE MARIKANI NI MUASISI WA MASHIRIKA YANAYOENDESHA UFISADI WA KIMATAIFA HAYA NI IMF NA WORLD BANK HII INADHIHIRISHWA NA RIPOTI YAO MBONA WAO HAWAIBIWI WENYE AKILI WANGEJIULIZA JEE MARIKANI NI WAADILIFU ??????? KAMA SI DANGANYA WAJINGA ILI KUPOTEZA MALENGO HII RESEARCH INGEFANYIKA CHINA ,RUSSIA AU NCHI YOYOTE YA KIJAMAA INGEINGIA AKILINI MWANGU NAONA NI UKOLONI MAMBOLEO NA UBEBERU AMBAO NI WACHACHEWENYE UFAHAMU NAO

    ReplyDelete
  12. NANI ACHAGUE HILI NDUNGAI JITU LINATUMIA MUDA WOTE KUTAMBULISHA WAGENI WA MAWAZIRI NA KUKANDAMIZA HOJA MUHIMU TOKA KWA WABUNGE ASIFIKIRI ATAULA KAMA BOSI WAKE HUUPATI NGO USPIKA CCM KIFO CHA MENDE 2015 HATA MIGIRO AKIGOMBEA URAIS HAMNA CHENU

    ReplyDelete
  13. Naomba niseme huyo Ndungai mtu muongo na mjinga sana,wabunge mara kwa mara wamekuwa wakisema bungeni,wakimtaja mtu ohoo siyo vizuri kutaja jina la mtu na ukimtaja mtu asiyekuwepo bungeni sheria haikuruhusu kwamba hawezi kujitetea kibunge.Na aliyepeleka taarifa hiyo anaambiwa atapelekwa kwenyekamati ya maadili ya bunge ajieleze.Gavana anasema wao hawanataarifa na hawajui chochote kuhusu hizo uwepo wa hizo pesa nje eti uswiss haijawaambia/kuwapa taarifa, Zitto kaonge ni kazi ya serikali kuchunguza au imuhoji ili wajue wapi pa kuanzia,ndungai anakurupuka na kidomo chake kichafu eti Zitto muongo.Ndungai aseme serikali ya uswiss ndo waongo kwani ndo walitoa taarifa za uwepo wa pesa hizo kwao na kama hazina mwenyewe basi ndungai aombe MWONGOZO uswiss kuomba hizo pesa zirejeshwe kama chenji ya rada ilivyo kuwa siyo kuleta u-CCM na ujinga ujinga bila kutafakari nini anchoongea,anadhani hilo litamsaidia kisiasa? kama natafuta kuwa spika asubiri pia aache upuuzi.

    ReplyDelete