22 August 2012

Kalunde yafanya kweli Idi Pili



Na Mwandishi Wetu

BENDI ya muziki wa dansi juzi ilikonga nyoyo za mashabiki wake katika onesho maalumu la sikukuu ya Idi ya Pili, ambalo lilifanyika katika hoteli ya Jangwani Sea Breez, Dar es Salaam.

Katika onesho hilo, bendi hiyo pia iliitambulisha albamu yake mpya ya Imebaki stori, ambayo inatarajia kutoka hivi karibuni.


Nyimbo ambazo zilitambulishwa siku hiyo ni Imebaki stori iliyobeba jina la albamu, Ulinipendea nini, Njoo tucheze, Cisee, Nilie na nani, Fungua na Ndoto.

Bendi hiyo ilianza kufanya vitu vyake kuanzia saa 10 jioni, huku kivutio kikuwa kikiwa kwa wacheza shoo, Queen Vero na Aminatha Othman.

Licha ya bendi hiyo kutambulisha albamu hiyo, pia ilipiga nyimbo zake zilizopo katika albamu ya kwanza ya Hilda, ambayo bado inafanya vyema katika anga za muziki wa dansi.

Akizungumzia maendeleo ya bendi hiyo, kiongozi wake Bob Rudala alisema kwamba hivi sasa wamejiapnga kuleta ushindani katika soko la muziki nchini pamoja na nje ya nchi.

"Kiukweli tumejipanga kikamilifu kuingia katika soko la muziki wa dansi na tuna imani tutafanya vyema kutokana na maandalizi tuliyofanya," alisema Rudala.

No comments:

Post a Comment