16 August 2012

CUF nao wamshukia Nnauye



Na Grace Ndossa

CHAMA cha Wananchi (CUF), kimedai kushangazwa na kauli iliyotolewa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Bw. Nape Nnauye kwa vyombo vya habari kuwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimeingia mikataba ya kifisadi na wafadhili wa nje ili kupora rasilimali za nchi.

Taarifa iliyotolewa Dar es Salaama jana na Naibu Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa CUF, Bw. Abdul Kambaya, alisema Bw. Nnauye hakupaswa kuishtaki CHADEMA kwa wananchi bali kupitia Serikali yao walipaswa kuzuia fedha hizo na kuwataja wafadhili hao.

“CUF kimeshangazwa na kauli hii ambayo imetolewa na msemaji wa CCM, ambacho ndio chama kinachoongoza nchi, tulitarajia Bw. Nnauye angewataja hao wafadhili wa CHADEMA ambao dhamira yao ni kupora rasilimali za nchi,” alisema Bw. Kambaya.

Aliongeza kuwa, chama hicho kinaamini CCM na CHADEMA ni watoto wa familia moja ambapo wafadhili wao ndani na nje ya nchi pia wa aina moja.

“Kama CHADEMA imeingia mikataba ya kupewa mabilioni ili baadae wataposhika madaraka waweze kulipa mabilioni hayo kupitia rasilimali za nchi basi watakuwa wanaendeleza utaratibu wa CCM kuingia mikataba mibovu isiyo na tija kwa Watanzania,” alisema.

Alisema CUF  inaamini kuwa, tatizo lililopo nchini ni mifumo mibovu inayoendesha Serikali, nchi, kukithiri kwa wizi, matumizi mabaya ya fedha za umma na ukiukwaji wa haki za binaadamu.

Bw. Kambaya alisema, sababu ya Watanzania wengi kuwa maskini wa kutupwa, ukosefu wa huduma bora kwa jamii, kudumaa kwa maendeleo ya nchi na ukosefu wa ajira ni matokeo ya muda mrefu yanayosababishwa na mfumo mbovu uliopo.

Alisema njia sahihi ya kulinda rasilimali zilizopo na zinazoendelea kugunduliwa nchini Serikali ya Umoja wa Kitafa ambayo itashirikisha vyama vyote vyenye wabunge.

Aliongeza kuwa, kwa kuzingatia utaratibu huo hakuna chama ambacho kitakuwa na maamuzi yake katika matumizi ya rasilimali na Maliasili za nchi.

“Sisi tunataka Watanzania waelewe kuwa, mazingira yanaonesha CHADEMA kimeizidi kete chama tawala kwa kuwa na wafadhili wa nje ndio maana CCM Inapiga kelele,” alisema.

2 comments:

  1. CHAMA CHOCHOTE CHA SIASA KAMA VILE CHADEMA, CUF,TLP, UDP,DPP N.K CHENYE NIA ZA DHATI ZA KUWAKOMBOA WATANZANIA KIUCHUMI NA KIMAENDELEO KINA HAKI KUCHANGIWA NA WANANCHI WOWOTE WAWE WA NDANI AU WA NJE YA NCHI. MIJINI NA VIJINI.

    WAKULIMA,WAFANYABIASHARA,WAFANYAKAZI,WANAFUNZI, WAJANE, MASIKINI, WAZEE N.K. WANALOJUKUMU LA KUVICHANGIA HIVI VYAMA. WANAWEZA KUCHANGIA FEDHA, KUKU, BATA, MAZAO, MALAZI,CHAKULA, MBUZI. USAFIRI, NGUO KWA WAPIGANIAJI WA HAKI NA UKOMBOZI WA WANANCHI. WENYE SHIDA NI WANANCHI NA INABIDI WAJICHANGIE WENYEWE KABLA YA KUOMBA MISAADA KUTOKA NJE. VYAMA VISITUMIE NJIA ZA MKATO ZA WIZI AU UJANJAUJANJA.

    MNAUYE AACHE KUWAHADAA WANANCHI. ASISAHAU KUWA ANAJIVUNIA SANA KUWA NA USHIRIKIANO NA ANC YA AFRICA KUSINI. ASIJILINGANISHE NA ANC KWA KUWA ANC HAIKUIBIA HELA AU KUCHOTA FEDHA KUTOKA SERIKALI YAO ILI KUKIENDESHA CHAMA CHAO. FEDHA WALIZOCHUKUA KIHALALI NI ZA WAWANANCHI AMBAZO MAKABURU WALIKUWA WAMEZILIMBIKIZA KUTOKANA NA JASHO LA WANANCHI WA S.A. HIVYO HIVYO, NYERERE WAKATI WA UCHANGA WA TANU,ILIBIDI ACHUKUE FEDHA ZA MKOLONI, MAKAMPUNI, VIWANDA, MNYUMBA N.K. ILI ZIENDESHE CHAMA NA SERIKALI ILIYOKUWA IMEACHWA MASIKINI. ANGEOMBA FEDHA UINGEREZA, USA, UCHINA AU URUSI HAWANAGALIMPA WAKATI HUO.

    BAADA YA HAPO MALI ZA SERIKALI ILIBIDI ZIWE ZA SERIKALI NA ZA CHAMA ZIWE ZA CHAMA.

    KINACHOENDELEA NI KUWA ccm IMEKUWA IKIIBA FEDHA KUTOKA SERIKALI KUJIENDESHA. MIFANO NI YA FEDHA ZA EPA, MASHIRIKA YALIYOKUWA MALI YA UMMA K.M. SIGARA, OXYGEN, BIA, BIMA,BANDARI, BENKI, NDC, TANESCO, MIFUKO YA HIFADHI ZA JAMII K.M NPF,NSSF, PPF N.K. WAFANYABIASHARA WLIKUWA WANATISHWA KUTOA MICHAANGO BILA HIARI YAO. CCM WAKIWAENDEA LEO HII, WATATOKA PATUPU BAADA YA WAFANYABIASHARA KUFUNGUKA.

    USHAHIDI UPO KWENYE MAHESABU. WAHASIBU WENGI WANAYAFAHAMU HAYA YOTE. WAHASIBU WANAFAHAMU NI BIA NA KANGA KIASI GANI TANU/CCM ILIKUWA INACHUKUA KUTOKA VIWANDANI HIVI BILA HATA KULIPA KODI. BIDHAA ZILIKUWA ZINAUZWA KWA WANANCHI KWA BEI YENYE KODI. HUU NI WIZI WA KODI ZA WANANCHI!

    USHAURI KWA NAPE AJIWEKE MBALI NA ANC. ASIWACHAFUE. DEEP GREEN NA KAGODA SIO WALIKUWA WAFANYE NA ANC BIASHARA? WANANCHI WAMEGUNDUA JANJA HII. MCHAKATO WA TENDA YA VITAMBULISHO VYA TAIFA SIO MOJAWAPO YA MBINU ZA KUTAFUTA 10% KWA AJILI YA CCM HADI UPINZANI ULIPOGUNDUA HUU UCHAFU?. NA FEDHA ZA VIBALI TUSAHAU! MATAIFA NA VYAMA VYA SIASA VYA NJE VIMEGUNDUA ULAGHAI WA CCM. BIASHARA ZA KAPINGA NA UCHINA KUPITIA CCM ZIMESAHAULIKA? CCM YA SASA INABIDI ILE KUTEGEMEA NA UREFU WA KAMBA YAKE. UJANJAUJANZA BASI!

    ReplyDelete
  2. NINGESHAURI UTAIFISHAJI PIA. MIKATABA YOTE ILIYOSAINIWA KWA KIPINDI HIKI NI AIBU> WENGI HAWALIPI HATA KODI, MASHIRIKA MENGI YA NJE NI FEKI NA NI MIKATABA YA MARAISI NA MAWAZIRI WACHACHE. KWA NINI MNASAINI MIKATABA INAYOMWIBIA MKULIMA< MFUGAJI, MWENYE ARDHI AMBAPO PANA MADINI.UNATOA ASILIMIA 90. na KUBAKI NA 10. HATA ASIYESOMA HAWEZI KUSAINI MKATABA WA KIPUMBAVU NAMNA HII. UNAAMUA WATU WACHIMBE ERANIUM KWENYE MBUGA ,HUJASOMA? UNAWEZA KUSOMA KWENYE INTERNET UKAJUA MADHARA YAKE. UNAWARUHUSU WAZUNGU KUCHUKUA WANYAMA NA NDEGE ZAO USIKU, UNAWAACHIA WAZUNGU WACHUKUE URANIUM KWA NDEGE KWA MIAKA MIWILI BILA KUNUFAISHA WATU> MNAWAACHIA WAZUNGU KUCHUKUA ARGHI MBUYULA < SONGEA VIJIJINI KWA BURE MKIJUA HAWA WATU BADO HAWAJAFUNGUA MACHO.MAENEO YOTE YA KUJIPAIA PESA KWENYE MBUGA ZA WANYAMA, SERENGETI< SELOU, NI WAZNGU NA WATU WAO WA AFRIKA YA KUSINI. SASA MNACHOJITETEA NI NINI< BILA AIBU, MBONA MNAIABISHA NCHI YETU, MNADHARALISHA WATU WOTE WA TANZANIA, NA, NAPE SIJUI ANAKISOMO NAMWAMKO WA NAMNA GANI.ZA MWIZI NI AROBAINI. SASA MKO NJE< SI HAPA NYUMBANI TU HATA KWENYE MAGAZETI YA NJE TUNASOMA. MLIMWONA RAISI WA MISRI ALIVYOTUMIKA< KUWALAZA WATU GIZANI , MNAKULA NAO< lAKINI WATAWAGEUKA TU. SABABU BADO WATATAKA UHUSIANO WA NCHI YETU. MNATOA UCHUMI WOTE NA KUWAACHA WATANZANIA GIZANI, BILA MAJI SAFI, BILA BARAR BARA< BILA HOSPITALI, BILA SHULE, . NYINYI MKIUMWA NJE. MTANZANIA AMECHOKA.MJITOE WOTE WENYE UCHAFU, MFUNGULIWE MASHTAKA, MALI ZENU ZOTE ZITAIFISHWE, NA MSIWE NA PASI ZA KUTOKA NJE.GEREZANI NI MASKANI YENU YAWANGOJEA>

    ReplyDelete