31 August 2012

CCM: Tunaweza kuifuta CHADEMA *Wassira awaonya kutovuruga amani nchini


Na Raphael Okello, Bunda

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu), Bw. Stephen Wassira, amesema Serikali ina uwezo wa kumuomba Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Bw. John Tendwa ili akifute Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kama kitaendeleza siasa za kuvuruga amani ya nchi.

Alisema Watanzania walikubali mfumo wa vyama vingi kwa nia njema ya kuleta demokrasia ya uhuru wa kutoa maoni na kulumbana kwa hoja bila kuvuruga amani, utulivu au kufanya uchochezi.

“Katiba ya nchi inatoa haki kwa vyama vyote vya siasa kufanya maandamano na mikutano ya hadhara kwa kuzingatia taratibu na sheria ya nchi badala ya kujiamulia na kufanya fujo,” alisema.

Aliongeza kuwa, uhuru wowote una mipaka yake kwani sheria hairuhusu kila mtu, kikundi cha watu au chama chochote kufanya wanavyoona inafaa na kutoa shutuma za kichochezi.

“Watanzania wanapaswa kuelewa kuwa, Seriokali ina uwezo wa kuipa CHADEMA kadi ya njano na kama itaendelea kucheza rafu uwanjani, itapewa nyekundu.

“Sisi tulipewa dhamana na wananchi ili kulinda amani, utulivu na
mshikamano wa Taifa, hatupo tayari kuvumilia vitendo visivyokoma vya kuvuruga amani na utulivu....tunaiomba CHADEMA waheshimu sheria ya mchezo vyama vingi,” alisema.


Bw. Wassira ambaye anafanya ziara ya kutembelea wapiga kura jimboni kwake, aliyasema hayo wakati akijibu maswali ya wakazi wa Kijiji cha Bukama, Kata ya Nyamuswa, wilayani Bunda.

Wakazi hao walitaka kujua Serikali kama walizni wa amani na utulivu wa nchi inaonaje mwenendo wa CHADEMA ambapo swali hilo liliulizwa na Bw. Samwel Msika, mkazi wa Kijiji cha Bukama.

“Wewe Bw. Wassira ni miongoni mwa viongozi Serikalini, hivi sasa umesema Serikali inahimiza amani, mshikamano na utulivu wa nchi, je mwenendo wa CHADEMA kufanya fujo mnauonaje ni salama, mmeukubali, mnauunga mkono au mnauzungumziaje,” alihoji.

Wakazi wengine wa kijiji hicho, walimtaka Bw. Wassira kutoa ufafanuzi juu ya kanuni za Bunge kama zinatoa fursa kwa wabunge kutoa maneno ya kashfa kwa kiongozi wa nchi.

Walidai ni hatua zipi ambazo zinachukuliwa kwa baadhi ya wabunge wanaotoa maneno hayo kwani wapo baadhi yao ambao hivi karibuni walifanya hivyo bungeni mjini Dodoma.

“Tunataka kujua msimamo wa Serikali na hatua zinazochukuliwa kwa baadhi wa viongozi serikalini pamoja na wabunge ambao hivi karibuni walidaiwa kujihusisha na vitendo vya rushwa na kuficha fedha za umma nje ya nchi,” alisema.

Akijibu hoja hizo, Bw. Wassira alisema pamoja na mambo mengine, kanuni na miongozo ya Bunge inakataza wabunge kutoa kauli za kashfa dhidi ya Rais na mbunge anayefanya hivyo, anachukuliwa hatua na Kamati ya Maadili ya Bunge.

Alisema zipo taratibu za kujadili utendaji wa Rais bungeni kwa Spika kupelekewa hoja badala ya kutoa maneno ya kashfa. Kuhusu mafisadi alisema uchunguzi unaendelea na wote ambao ushahidi wao utapatikana watashtakiwa.

Aliongeza kuwa, Serikali imekuwa ikichukua hatua ambapo hadi sasa, wapo baadhi ya Mawaziri ambao wamefikishwa mahakamani akiwataja Bw. Daniel Yona na Bw. Bazir Mramba na kuhadharisha wananchi kutofanyia kazi uzushi na chuki binafsi za wanasiasa.

21 comments:

  1. wasira ni waziri wa serikali dhalimu ambayo inatumia dola kuwapiga wananchi risasi za moto. hii nchi ni yetu sote kwa hiyo aache kuongea kama vile sis ni wageni na wao ndio wenye nchi. kwanaza hao waliouliza maswali walichomekwa kuuliza hayo maswali ya kichokonozi. acha hasira wassira- wewe utapita likini tanzania itabaki. tafakari

    ReplyDelete
  2. Wassira ifuteni kwanza CCM kabla ya chadema, kwani vurugu zote chanzo ni CCM hawataki kuachia madaraka

    ReplyDelete
  3. mmepotoka,futeni muone! ifuteni kwanza ccm kwani umaskini wote huu wa watanzania nyinyi ndo wahisika ili hali nyinyi ni mabilionea. au mnafikiri sisi hatujui? mnataka amani ili muendelee kutiuibia na kula kwa raha zenu sio? no no no!
    .

    ReplyDelete
  4. JAMANI HILI ZEEE LINA NINI KIPYA KAZI KULALA TU BUNGENI,UMEEZEEKA UMRI MPAKA AKILI, WAACHIE VIJANA

    ReplyDelete
  5. We mzee kama umechoka kazi kaa nyumbani usubiri kufa. CCM ni chama cha wezi na vibaka hatukitaki mnatuibia sana mkifute chadema ndo tutawaonyesha ka sisi ni nani

    ReplyDelete
  6. NI KAWAIDA YA CCM KUWEKA MIZEE ILI KUWATISHA VIJANA NDANI YA CCM NA TAIFA . ZEE HILI KAMA KINGUNGE , JAMANI TANZANIA YA 47 SI YA LEO VIJANA WOTE TUNATAKA MABALIKO BILA YA KUJALI ITIKADI YA VYAMA VYETU
    TANZANIA HOYEEEEEEEEEEE
    MIZEEEEEEEEEEEE TUACHIENI VIJANA

    ReplyDelete
  7. Naomba nizungumzie kidogo kuhusu hali ya kampeni inavyoendelea hapa nchini hasa kuhusu uchaguzi wa mwaka 2015.

    Kwa hali ambayo siyo ya kawaida tangu kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vyingi hapo mwaka 1992 tulishughudia utitiri wa vyama na tuliona jinsi upinzani ilivyoanza kwa nguvu chini ya chama cha NCCR Mageuzi kilichoongozwa na Mheshimiwa Mrema

    Lakini baada ya uchaguzi wa mwaka 1995 na CCM bado kuendelea kuwa madakani chama cha upinzani cha Chadema kilianza kupata nguvu Lakini tangu chama hiki kichukue nafasi ya kwanza kwenye upinzani tumeshughudia vifo vingi vilivyotokea kwa ajili ya siasa kabla hata hakijaingia madarakani. Siwezi kuelewa tofauti iliyokuwepo kati ya uongozi wa chama cha NCCR Mageuzi ambacho hakikumwaga damu na chama hiki cha Chadema.

    Lakini hoja yangu kubwa hapa ni kwamba serikali inatakiwa kuangalia kwa undani kwanini haya yanatokea kwanini watu wanauana ni kwa ajili ya chuki gani zilizoanzishwa na baada ya kugundua hilo serikali ilifanyie kazi badala ya kuendelea kulaumu chama cha upinzani.

    Tujifunze kwa wenzetu wa nchi za magharibi na mashariki kuwa hawana utitiri wa vyama, tangu kuanzishwa mfumo huu wa vyama vingi ni miaka 20/ishirini ,kijana aliyezaliwa mwaka 1992 yupo chuo kikuu lazima kuwe na mabadiliko /changes na serikali isiogope mabadiliko

    Serikali kama za Marekani na baadhi ya nchi za Ulaya zina vyama viwili mfano USA Republican na Democratic, serikali za England zina vyama vya labor na conservative, na baadhi ya nchi nyingine za Ulaya.

    Maana ya kuwa na vyama viwili kwanza ni kupunguza ruzuku inayokwenda kwenye vyama , Tanzania ina vyama zaidi ya 13 kila chama kinataka ruzuku toka kwenye fedha za walipa kodi , fedha hizi hizi zinatakiwa kwa maendeleo ya nchi.

    Katika utitiri huo CCM bado ina nafasi kubwa ya kushinda kwani ina mizizi imara tangu vijijini , wananchi wengi wa vijijini hasa wazee hawajui hata kama mwalimu Julius alishakufa na bado hawapo tayari kuhahama CCM

    Kwa maana hiyo serikali inatakiwa ikubali mabadiliko / changes na kupeleka bungeni hoja ya kuwa na vyama viwili tu vya siasa ili kuwapa wananchi nafasi ya kuchagua ni kipi kati ya hivyo na viwe na majina tofauti ili kuondoa upendeleo na na kupunguzi kodi inayokwenda kwenye vyama ya bure

    Aidha nafasi ya msemaji wa chama na msemaji wa serikali ndani ya chama ziangaliwe upya ifahamike nani msemaji wa serikali kwani kama hoja hii ya kukifuta chama cha upinzani ingetakiwa izungumzwe labda bungeni ili kupunguza fujo zinazoweza kutokea upande wa pili

    Kwa maoni yangu haya yakifuatwa basi tutakuwa na vyama vinavyojiheshimu vyenye kujenga hoja na kutatua matatizo ya wananchi.

    Tunajua kama chama kitashindwa kutekeleza sera zake wananchi watakihukumu katika uchaguzi unaofuata na hawatakichagua

    Tujifunze kutoka Marekani kupeana zamu miaka minne ya Democratic au Republican sasa hivi mheshimiwa Raisi Obama anapigania chama chake kishinde awamu ya pili kwa sera alizoziweka zimekubaliwa amezitekeleza na kupokelewa na wananchi basi watamchagua la sivyo mwakani itakuwa Raisi toka Republican

    Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ndugu mchangiaji hapo juu, Napata mashaka kuamini kua,umeweza kupata muda wa kuandika makala yako fupi bila kufanya utafiti kwa undani unachotaka kukizungumzia na hivyo kukuona kama mtu aliyekurupuka... Hebu tukupe nafasi ya pili ukafanye utafiti tuone kama hivyo ulivyoviandika mathalani kua vyama viwili utabadili mtazamo wako.. Umezungumzia suala la NCCR- MAGEUZI, ninaomba nikuulize NCCR-Mageuzi ikuapi leo hii, nitajie hata ofisi unazozifahamu za Nccr-mageuzi,. moja kati ya vyama vikongwe vilivyoasisiwa na kuongozwa na watu mashuhuri sana hapa nchini nikuulize wako wapi watu hao..? Chama hicho kiko wapi, viongozi wa taifa wameendelea kuwatumia watanzania kama mtaji na wao wakipata kutorosha mabilioni ya fedha kupeleka katika nchi za ulaya ilihali barabara hazipitiki nchini, Dar es salaam wanatekeleza miradi ya barabara iliyotakiwa itekelezwe karibu miaka kumi iliyopita na hivyo kuufanya mradi kutokwenda na wakati, zikuwapi hadithi za treni Kama chombo cha usafiri DAR ES SALAAM.? Badala yake tunasikia hadithi za watendaji wakuu wa serikali kutafuna miradi na mitaji mbalimbali ya taifa hili tazama viwanda tulivyokua navyo kama hicho cha matairi Arusha ambacho sasa kimetelekezwa wakati ndicho katika miaka ya themanini kilichokua kikiongoza kwa uuzaji wa matairi Afrika mashariki na kati.. ni dhahiri kua NCCR-MAGEUZI, Walishindwa kututoa kwenye mikono ya CCM na kuleta mabadiliko halisi tunayoyahitaji, na niwe mkweli hapa nathamini sana mchango wa NCCR-MAGEUZI katika kukuza siasa za vyama vingi hapa nchini. lakini ifike wakati tujifunge mikanda kutetea na kupigania maisha yetu ya baadaye na ya vizazi vijavyo.

      Delete
  8. wewe mchangiaji ics;
    acha kupotosha kama babu yako wassira,nani kakuambia USA wana vyama 2 tu siasa?au ni nani kakudanganya kuwa UK kuna vyama 2 tu?hao watu unaosema wameuawa wakati chadema kikiwa chama kikuu cha upinzani,waliuliwa na chadema?try to use ur brain

    ReplyDelete
  9. ics upeo wake wa kufikiria ni mdogo hivyo siwezi kumshangaa. shida yake ni uoga na ni mmoja kati ya watu ambao huwa hawezi kufikiria na kazi yake ni kuzungumzia waliofikiria wenzake,yaani wafikirie wenzake yeye naye apite humu humu

    ReplyDelete
  10. kasahau ya zanzibar kijana huyo na kuhusu Uk na USA kuna vyama vingi sema vyenye majina ni 2 tu ila uliza Uk, chama gani kiliungana na green part ili kuunda serikali

    ReplyDelete
  11. Kukifuta CHADEMA hakutaziba midomo ya watanzania kupiga kelele juu ya umaskini ambao unasababishwa na rushwa,wizi,ulafi,ufisadi na kila aina ya uovu unaofanywa na serikali ya CCM.Kama hawawezi kuona CCM ikibadilika kwa kuachana na uovu huo lazima watafute mbadala.
    Hayati baba wa Taifa Mwl.J.K.Nyerere alisema,Watanzania wanataka kuona mabadiliko ndani ya CCM,wasipoyaona watayatafuta nje ya CCM.
    Kwa kuwa sasa watanzania hawawezi kuyaona mabadiliko ndani ya CCM, wanayatafuta ndani ya vyama vya upinzani.Ni vizuri tu CCM wakajiandaa kisaikolojia kabla ya kukabidhi dola.Dawa si kuua wala kukifuta CHADEMA.
    Mwisho, CCM wajue kila damu isiyo na hatia ambayo wanaimwagwa Mungu ataitaka juu ya vichwa vyao.Wasifikiri eti wako salama, wanajidanganya.

    ReplyDelete
  12. Mzee Wasira...Mzuka wako ndio unaweza kuifuta CDM!
    Ni vizuri nyote wewe, Nchimbi na wengine wenye mawazo kama ya kwako kwamba SERIKALI YENU NA CHAMA CHENU CCM NDIO MNAYOLETA FUJO KWA MAKUSUDI NA KUSABABISHA MAUAJI YA WATANZANIA MASIKINI. kama mnataka kuona hilo ruhusuni CHADEMA na vyama vingine vyovyote vifanye mikutano na maandamano halafu MUWAWEKEE SHARTI LA USALAMA KWENYE SHUGHULI ZAO MUONE KAMA HATA MTU MMOJA ATACHUBUKA! TUNA TAARIFA KWAMBA NI MKAKATI WA CCM NA SERIKALI KUIFANYA CHADEMA IONEKANE CHAMA CHA VURUGU, HILO MJUE HALITAFANIKIWA KWANI LIMESHAFAHAMIKA NA MBINU ZENYEWE NDIO HIZO. MNAENDA NA MABOMU YA KIVITA KWENYE KUTAWANYA WATU HATA 100 HAWAFIKI,KAMA SIO KIWEWE NA WENDAWAZIMU NI NINI? JARIBUNI KUTAMBUA KWAMBA WATU WAMEWACHOKA, KILAMNALOFANYA LINAFAHAMIKA, ACHENI DEMOCRASIA ICHUKUE MKONDO WAKE!!

    ReplyDelete
  13. si serikali itaomba, aseme ccm itamuomba mwana ccm waliyemweka la sivyo atatolewa katika nafasi yake akitaka kujifanya anajua maana ya democrasia. Wasira anataka atupelekeshe na kutufanya sisi watoto wadogo hata tusiweze pata yale mabaya na ubabe waufanyao?

    ReplyDelete
  14. "Killing and Compassion are the last thing that a Leader has to learn". Imefika wakati sasa hawa viongozi wetu wa kisiasa wakae chini na kujiuliza siasa za uaji ndiyo siasa ya amani,upendo na utulivu katika kuijenga Tanzania hii. Ila nasi wananchi tunapaswa kujiuliza....sisi wananchi tunauwawa na kuvurugana kwa ajili ya vyama wanavyo viongoza wao; wakati wao wana keti na kutupiana maneno ya kashifa za kisiasa kwenye vyombo vya habari je hili kweli litatusaidia sisi wananchi kwa kuamini kwamba fulani ndiyo bora na chama anacho kiongoza? Hembu tutafakari hii siasa ya umwagaji damu kama kweli inatija kwetu kwani "All that glitters is not Gold".

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mbona ewe mtanzania sikuelewi unaposema "siasa za umwagaji damu" swali langu hivi siasa ndiyo inamwaga damu? naomba mifano. Nijuavyo mimi polisi ndio wamwagaju damu na sasa watu wanawaogopa polosi na si vyama vya siasa. Mfano aliyeuwawa Nyololo aliuwawa na polisi na si chama, Morogoro hali kadharika, nk.

      Delete
  15. Huyu mjinga ! chama cha kuftwa sio kingine bali ni CCM ,
    Babu mzima ana wanawake watatu na watoto utitiri, kazi ya kujenga taifa anafanya saa ngapi..
    Na kubwa zaidi yeye ndiye mshauri wa rais -- shida na kero zote na maamuzi mabaya ya rais.. yeye yuko behind ! Mbuzi kabisa na huyo mjomba wake warioba .. kwanza nashangaa hawa watu ambao computer wanadhani ni redio..ni kizazi cha miaka ya 1930! nani anawahitaji ? Julius Nyerere aliwaomba viongozi wazee wang'atuke na kung'atuka ni neno la kabila lao ..hawajui kung'atukaaa...Pambaafuu sana (( wanaudhi hadi nashindwa kukontrol hasira zangu ) Morogoro wameua muuza gazeti, Ulimboka kanusurika , iringa wameua kama mbwa ,, Ni chama gani kifutiwe usajili... fuck CCM.. Fuck the so called waheshimiwa ! nashangaa hata kuwaita waheshimiwa ! utamheshimu jangili , muuaji , mwizi ,ebu acheni ...mimi mwenye uchungu na maneno ya wasira nasema Fuck u wasira

    ReplyDelete
  16. Nashindwa kuamini maneno ya huyu mdudu anayeitwa Wassira na huyu aliyeposti maoni kwa jina la icc kama niwatu wenye akili timamu au ni mashine tu.
    Wassira anazungumza kanakwamba uwepo wa CHADEMA na vyama pinzani ni kwa ukarimu wa chama chake cha wezi, vibaka, majangili, wazushi, waongo nawauaji - CCM. Ana maradhi ya kusahau sahau huyu, maana angukuwa fit angekumbuka hata TANU haikuanzishwa kwa kupewa ridhaa ya Mkoloni. Hafahamu kwamba wenye uwezo wa kukifuta chama ni wananchi na si wezi hawa kina Wassira na wenzake waliolifanya taifa hili lipige magoti kwa umasikini ulioletwa na ulafi wao. Wametuibia, wametufilisi, wametuteka nyara na kututesa, wametumia sumu kuwanyamazisha wenye mawazo tofauti na wao, wamuetujeruhi, wanatuua kama paka au mbwa na waanatamani kututawala kwa fimbo ya chuma milele. Hata punda akizidiwa anakaa chini; na sisi kamwe hatutakubali kutumika kama wanasesere ili kunenepesha matumbo yao. Wajaribu wakifute CHADEMA ili waiingize nchi katika matatizoyaliyomfanya mkoloni mwenzao Mwingereza kusalimu amri. Mwingereza alikuwa na pa kukimbilia - kwao Uingereza, hawa manyag'au watakimbilia wapi?

    ReplyDelete
    Replies
    1. HATARI... SIASA ZA KUFIKIA HAPO TOOOOOO MUCH, BINADAMU KUMWITA MDUDU (NI SIASA, USHABIKI AU HASIRA ZA BILA BUSARA?)

      Delete
  17. kuifuta chadema sio suluhisho la kunyamazisha watanzania.hamuwezi kuona kwamba suala hapa ni kuwa watu wamechoka na si suala la chama.ukifuta chadema itakuja chaduma na itakuwa vile vile.

    ReplyDelete
  18. hivi hawa viongozi wetu wemelewa\ sana madaraka waliofanya fujo na kuua watu ni polisi ,kama chadema ndio wangekua wamefanya fujo si wangekufa polisi waifute polisi nayo

    ReplyDelete