17 July 2012

Watanzania washindwa kutokea ZIFF



Na Amina Athumani, Zanzibar

TAMASHA la 15 la filamu kwa nchi za Majahazi  la Zanzibar International Film Festival (ZIFF), limemalizika juzi lakini wasanii wengi wa Tanzania wameshindwa kujitokeza.

Wasanii wengi wa Tanzania hasa wa Bongo Movie, wameshindwa kujumuika pamoja na wenzao katika tamasha hilo na kutoa nafasi kwa filamu za nchi mbalimbali kutwaa tuzo nyingi.

Katika usiku wa kutoa tuzo uliyosheheni wasanii wa nje, takriban tuzo tano kubwa zimekwenda Afrika Kusini kupitia filamu ya Uhlanga.

Tanzania kama kawaida imepata tuzo katika nafasi ya upendeleo, ambapo tuzo yao haikugombewa na filamu yoyote kutoka nje.

Tuzo hiyo ni ya filamu bora ya Kitanzania, ambayo imekwenda kwa filamu ya Chungu pamoja na muigizaji bora iliyokwenda pia kwa muigizaji wa filamu hiyo.

Tuzo nyingine zilizokuwa zikiwaniwa katika tamasha hilo ni zilizotolewa na wadhamini wa tamasha hilo ZUKU (ZUKU Award) ambazo ni  filamu bora ya Afrika ambapo filamu ya Inside Stori ya Afrika Kusini ilishinda na muigizaji bora wa Afrika iliyochukuliwa na Kelvin Ndege kutoka kwenye filamu hiyo.

Tuzo ya muigizaji bora wa kike Afrika ilikwenda kwa Thuli Khulamelo, Nomfundo Dunazana na Reona Ngiba wote kutoka Afrika Kusini kupitia filamu ya Uhlanga.

Kwa upande wa tuzo zilizotolewa na ZIFF zilikuwa ni filamu bora fupi iliyokwenda kwa Moccasing ya Kenya, Besti Documentary iliyokwenda kwa marehemu Miriam Makeba kupitia filamu ya Mama Afrika kutoka Afrika Kusini na Best Animation iliyokwenda kwenye filamu ya Ostora  ya nchini Syria.

Pia zilikuwepo tuzo ya best Feature Film  iliyokwenda kwa filamu ya Uhlanga, Zamora ya Tanzania na muigizaji bora wa Tanzania ikienda kwa Richard Mshanga.

Mbali na tuzo za ZIFF, pia kulitolewa tuzo mbalimbali za kimataifa ambapo tuzo ya Ousumane Sembene ilikwenda kwa filamu ya Uhlanga, tuzo ya Signis pia ilikwenda kwa Uhlanga na tuzo ya Verona ikienda pia kwa Uhlanga ya Afrika Kusini.

Kwa upande wa tuzo za heshima zilizotolewa na ZIFF, zilikwenda kwa Martin Mhando na Fabrizio Colombo.

Msimu huu ni wa 15 tangu kuanzishwa kwa tamasha hilo za ZIFF, ambapo awali lilikuwa likijulikana kama tamasha la nchi za Majahazi ambapo tuzo zilianza kutolewa mwaka 1874 na mwaka 1950, zikaanza kutoka rasmi kwa wasanii

No comments:

Post a Comment