16 July 2012

...Watakiwa kuchagua viongozi makini



Na Andrew Ignas

UONGOZI wa Yanga, umewataka wanachama wa klabu hiyo kuhakikisha wanachagua viongozi makini watakaoiletea maendeleo ya soka pamoja na kukuza uchumi.

Klabu hiyo leo inafanya uchaguzi mdogo kujaza nafasi zilizoachwa wazi na baadhi wa viongozi waliokuwepo akiwemo Mwenyekiti wake, Lloyd Nchunga.


Uchaguzi huo ambao wagombea watajaza nafasi Mwenyeki, Makamu Mwenyekiti na Wajumbe wanne utafanyika kuazia asubuhi katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam.

Akizungumza Dar es Salaam jana, mmoja wa wanachama wa Yanga, Bakili Makele alisema
anawaomba wanachama wenzake kufanya maamuzi makini kwani kwa kuchagua wababaishaji watakuwa hawajafanya kitu.

"Soka la sasa ni kama biashara, bila kupata viongozi makini ambao watakuwa na uwezo wa kujitolea kutoa fedha zao wenyewe kwa maendeleo ya klabu yetu, tutashindwa kufikia malengo yetu tuliyojiwekea," alisema.

Alisema klabu hiyo ina uwezo wa kukuza kichumi wake kama itapata viongozi watakaopigania maslahi ya wachezaji na klabu kwa ujumla bila kujiangalia wenyewe.

"Na imani Yanga inaweza kukuza uchumi wake kama kweli itapata viongozi wenye uchungu wa maendeleo ya klabu pamoja na wachezaji, lakini kama tutapata wababaishaji tutakuwa hatujatatua tatizo," alisema.

Makele pia aliwataka wanachama klabu hiyo kuwa watulivu katika uchaguzi huo wa leo na kuufanya kwa amani ili kudumisha mshikamano uliopo sasa

No comments:

Post a Comment