11 July 2012

Wananchi tusiupe nafasi umaskini wa fikra ili kuchochea maendeleo



UMASKINI katika jamii ya Watanzania si msamiati mgeni hasa wakati huu ambao kumekuwepo na jitihada mbalimbali za kitaifa na kimataifa kuuangamiza.

Inaelezwa kuwa, ili mtu apate mafanikio katika tatizo linalomsibu, lazima  ajitambue hivyo kila anayeshiriki kutokomeza umaskini anapaswa kujua maskini ni nani?

Kuna vipimo viwili vya kumtambua maskini, kwanza kipimo cha kimataifa ambacho kinasema “Mtu yeyote anayepata kipato chini ya dola moja kwa siku, anahesabika ni maskini”

Kipimo kingine hutumiwa na wataalamu wengi wa uchumi cha kujipatia mahitahi ya lazima ambayo ni chakula, malazi na mavazi.

Kwa upande wa chakula, huangaliwa uwezo wa kaya kumudu milo mitatu kwa siku, kama hawapati, huesabiwa ni maskini. Katika malazi, huangaliwa nyumba wanayoishi familia husika.

Kama haina faragha wala choo, wanajibanza kwenye chumba kimoja au wanalala na mifugo, familia hiyo huitwa maskini wa kutupwa. Mavazi nayo hutumika kama kipimo cha kumtambua maskini.

Familia zinaposhindwa kuwa na nguo safi, zinazofuliwa kila mara na kunyooshwa, huingizwa kwenye kundi la watu maskini hivyo ni wazi kuwa, familia zinapokosa kipato na mahitaji ya lazima, hukosa ziada ya elimu ya watoto, afya na maji safi.

Tanzania ni miongoni mwa nchi maskini ambayo hupimwa kutokana na uchache wa pato la taifa kwa mwaka, matumizi ya kiwango cha chini cha teknolojia, uduni wa huduma za jamii, miundombinu hafifu,  madeni, upatikanaji wa maji safi na salama, uwezo mdogo wa kuzalisha katika sekta ya kilimo na viwanda.

Kutokana na vipimo hivyo, Taifa na watu wake ni maskini lakini tunapaswa kujiuliza, tangu uhuru kwanini tunashindwa kupunguza umaskini.

Sisi tunasema kuwa, moja ya sababu inayokwamisha kuondoa umaskini ni mtazamo, umaskini wa fikra unawafanya Watanzania wengi kuogopa kuingia katika shughuli za maendeleo.

Kwa mfano, mtu ana shamba kubwa lenye miti badala ya kupata utaalamu wa kufuga nyuki ili azalishe asali, anaona bora anunue shoka ili akate mkaa.

Ukataji mkaa ni sulba kubwa, haina tija na kipato chake ni kidogo
ambapo kubadili fikra, kunakuja baada ya kujitambua, watu wengi hufikiria umaskini ni maumbile.

Mara zote  mara zote vita ya kupambana na umaskini hufanywa kwa mazoea. Umaskini wa fikra husababisha wananchi kutokujitambua na kutambua mustakabali mzima wa maisha yao.

Wengi hukosa upeo wa utambuzi jambo ambalo husababisha kutopata tija au ufanisi kidogo katika shughuli za utafutaji riziki

No comments:

Post a Comment